Nay wa Mitego Atangaza Mali zake, Yamo Majengo na Magari..Adai kwa Sasa Yupo Single - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Atangaza Mali zake, Yamo Majengo na Magari..Adai kwa Sasa Yupo Single

STAA wa Bongo Fleva nchini, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuhusu mali zake anazomiliki.

Nay ameyafunguka hayo wakati akihojiwa katika Kipindi cha Sporah kinachoruka kupitia Runinga ya Clouds TV kila Jumanne usiku.

Staa huyo amesema anamiliki nyumba tatu, magari matatu ambayo ni Toyota Prado, Nissani Murano na Toyota Passo.

Mbali ya vitu hivyo pamoja na muziki, pia staa huyo anavitega uchumi ambavyo vinamuingizia kipato ikiwemo bajaj, saluni na vinginevyo.

Kwa upande wa mahusiano, Nay amesema kwa sasa yupo ‘single’ akiwalea watoto wake wawili baada ya kutofautiana na mpenzi wake wa tatu Siwema na kuamua kumchukua mtoto wake mchanga anayedai alikuwa hapati malezi bora kutokana na mama yake huyo kuwa bize na biashara zake.

Nay ameeleza historia ya mahusiano yake akiweka wazi wapenzi wake watatu ambao amezaa nao watoto akianza na wa kwanza ambaye alikuwa Mhindi huku wa pili akiwa msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ kabla ya kumaliza na Siwema ambaye wametofautiana hivi karibuni.

Nay amesema kwa sasa ana watoto watatu ambao aliwapata na wapenzi wake hao watatu wa zamani na kati ya hao wawili anaishi nao.

Lakini mbali na kusema kwa sasa yupo single, staa huyo hivi karibuni amekuwa na uhusiano wa karibu sana na mwigizaji wa filamu za Kibongo Shamsa Ford huku wakipiga picha kadhaa za kimahaba na kuziachia mitandaoni.

Kuhusu muziki, Nay amefunguka kuwa yeye anafanya muziki biashara akiangalia soko la muziki linataka nini ili aweze kuendelea kuwa juu.

Mipango yake katika miziki ni pamoja na kufanya kolabo mbalimbali na mastaa wa nje akiwemo Wizkid na D’banj na wengineo ambapo baadhi yao tayari amenza kufanya nao kazi.

Kwa upande wa hapa Bongo, Nay amesema anatarajia kutoa ngoma nyingine ambayo amefanya na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz huku akiongeza kuwa atafanya pia kolabo na wasanii wa kike ili kuboresha muziki wake na kuwapa raha mashabiki wake
GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.