MANNY PACQUIAO KUSHTAKIWA KWA UDANGANYIFU - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MANNY PACQUIAO KUSHTAKIWA KWA UDANGANYIFU

Bet Sasa
Bondia Manny Pacquiao anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushindwa kuorodhesha taarifa za maumivu ya bega kwenye fomu maalum kabla ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather mwishoni mwa juma lililopita.
Manny Pacquiao Kushtakiwa Kwa Udanganyifu

Pacquiao anaweza kuwa nje ya ulingo kwa zaidi ya miezi tisa, wakati anajiandaa kwenda kufanyiwa upasuaji wa bega baada ya kuumia mazoezi akijiandaa na pambano hilo.

Ushahidi wa nakala ya fomu iliyotakiwa kujazwa na bondia huyo kutoka Ufilipino umetolewa na inaonyesha katika kipengele cha majeraha hakikujazwa huku ikionyesha Pacquiao alitumia dawa kadhaa za maumivu.

Sehemu muhimu inayothibitisha uweli wa jambo hilo imezunguushiwa mstari mwekundu kwa ushahidi, ambapo swali liliuliza; ‘Ulikuwa una maumivu yoyote kwenye mabega yako, chini ya mabega, au mikononi ambayo yanahitaji vipimo vya uthibitisho wa kupona?’


Nakala ya fomu ya maelezo muhimu ya Pacquiao kabla ya pambano haikuorodhesha maumivu ya bega lake

Kwa kusaini fomu hiyo, wote Pacquiao na mshauri wake Michael Koncz wanaweza kuchukuliwa hatua kwa sababu, mwishoni kuna maelezo yasemamo; “Maelezo ya hapo juu ni kweli na sahihi nikiwa na akili zangu timamu,”

Adhabu ya kosa hilo kwa kawaida huwa ni kufungwa jela kati ya mwaka mmoja mpaka minne na kutozwa faini ya dola za Kimarekani 5,000 (Sh. Milioni 20).

Pacquiao anaweza pia kutozwa faini na kufungiwa na Kamisheni ya Michezo Nevada.

Mwenyekiti wa Kamisheni, Francisco Aguilar amesema kwamba ofisi ya Mwanasheria Mkuu itachunguza kwa nini maumivu hayo hayakuorodheshwa.

“Na tutafanya majadiliano fulani. Kwa sababu Kamisheni inapaswa kupata maelezo ya kila wakati ya bondia.

Tiba aliyopata iliorodheshwa kwenye fomu, lakini si ya maumivu halisi. Hili si pambano letu la kwanza. Hii ni biashara yetu. Kuna utaratibu, na unapojaribu kukiuka utaratibu, hatuwezi kufanya kazi na wewe,” alisema Francisco Aguilar.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.