Chris Brown Apata msala Mwingine, ni wa kumpiga mtu ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chris Brown Apata msala Mwingine, ni wa kumpiga mtu !

Chris Brown ameunusa tena mtungi wa sheria. Staa huyo wa R&B anachunguzwa kufuatia tukio la kupigwa mtu lililotokea Jumatatu hii kwenye hoteli ya Palms Casino Resort, Las Vegas.
LOS ANGELES, CA - JUNE 28:  Singer Chris Brown attends the Sprite Celebrity Basketball Game during the 2014 BET Experience At L.A. LIVE on June 28, 2014 in Los Angeles, California.  (Photo by Noel Vasquez/BET/Getty Images for BET)

LOS ANGELES, CA – JUNE 28: Singer Chris Brown attends the Sprite Celebrity Basketball 
Game during the 2014 BET Experience At L.A. LIVE on June 28, 2014 in Los Angeles, 
California. (Photo by Noel Vasquez/BET/Getty Images for BET)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa Las Vegas, polisi walipokea simu kutoka hospitali ya Sunrise ambapo mwanaume mmoja alikuwa akitibiwa kwa majeraha ya kawaida kutokana na kupigwa.
Brown alikuwa akicheza kikapu kwenye hoteli hiyo na kuanza kurushiana maneno na mtu waliyekuwa wakicheza naye na kuzuka ugomvi wa ngumi. Mtu huyo amedai kuwa alipigwa ngumi na Brown na wakati anajitetea alipigwa na mtu mwingine anayedaiwa kuwa upande wa Brown.
Kwa mujibu wa mtandao wa ThisIs50, Brown alikuwa akicheza kikapu na muimbaji mwenzie Jeremih ambapo baada ya timu ya Jeremih kushinda kukafanyika mechi ya marudiano na ndipo ugomvi ulipozuka.
Polisi walishindwa kuzungumza na Brown walipowasili kwenye hoteli hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.