Chelsea Ndio Wafalme Wapya England Kwa Sasa…Jionee Ma Photos ya Shangwe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chelsea Ndio Wafalme Wapya England Kwa Sasa…Jionee Ma Photos ya Shangwe

chee
Ushindi wa bao 1-0 kwa Chelsea dhidi ya Crystal Palace umeitangazia ubingwa klabu hiyo na sasa ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya England.
ubi
Kwa ushindi huo, Chelsea imefikisha pointi 83 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi hiyo.
ubing
Kabla ya mchezo wao wa jana mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Dider Drogbaalionyesha hisia zake za kutaka kufunga katika mchezo huo ili kuhitimisha ubingwa wao lakini bahati haikuwa yake na badala yake bao pekee la ushindi lilifungwa na Eden Hazard.
fab
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge maarufu kama darajani, Chelsea walipata bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao Eden Hazard ambaye alipiga mkwaju wa penalti ukaokolewa na kipa lakini mpira ukamkuta tena yeye na kumalizia kwa kichwa.
chelsea
-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.