Bondia Manny Pacquiao Hatopanda Ulingoni Kwa Zaidi Ya Miezi 9. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bondia Manny Pacquiao Hatopanda Ulingoni Kwa Zaidi Ya Miezi 9.Kwa mujibu wa toviti ya ESPN bondia huyo alipambana na Maywaeather huku akiwa na maumivu makali ya bega.
Vipimo vya MRI alivyofanyia Pacquiao, mara baada ya pambano hilo vimeonyesha anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje ya ulingo kwa muda wa miezi tisa hadi kumi na mbili.
Hata hivyo ilidaiwa kwamba, Pacquiao alidhamiria kujiondoa katika pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lililofanyika May mbili, lakini ombi lake lilikataliwa na kamisheni ya michezo ya Nedava, na pia alinyimwa nafasi ya kuchoma sindano ya ganzi kabla ya kupanda ulingoni ili kupunguza maumivu.
Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Pacquiao, hakufanya mazoezi kwa siku kadhaa kutokana na maumivu ya bega ambayo aliyatonesha kutokana na maandalizi makali ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.