Baada ya Manny Pacquiao kushindwa pambano dhidi ya Mayweather, ametoa kauli hii hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Manny Pacquiao kushindwa pambano dhidi ya Mayweather, ametoa kauli hii hapa

Manny Pacquiao reacts after his fight against Floyd Mayweather Jr. in a welterweight unification bout on May 2, 2015 at the MGM Grand Garden Arena in Las Vegas, Nevada. AFP PHOTO / FREDERIC J. BROWN        (Photo credit should read FREDERIC J. BROWN/AFP/Getty Images)
Manny Pacquiao amepingana kwa nguvu zake zote na matokeo ya pambalo lake dhidi ya Floyd Mayweather Jr kuwa ameshindwa pambano hilo la welterweight. 
Floyd Mayweather amemshinda Manny Pacquiao katika pambano hilo ambalo watu wengi wanadai kuwa maamuzi yalikuwa ni ya kutatanisha.

Pacquiao kwa upande wake anasema majaji watatu wa pambano hilo hawakutoa maamuzi sahihi
"Mimi nilidhani nimeshinda pambano, mimi sikuona kama Mayweather alifanya chochote kile kwangu, nilimpelekea makonde mara nyingi zaidi huku yeye muda mwingi akitumia kupanchi," Pacman alisema. "Nilimshambulia mara nyingi zaidi."

Pambano hilo ambalo limepewa sifa kama pambano la karne lilifanyika katikaukumbi wa MGM Grand arena uliopo Las Vegas.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.