Uwoya "Nimeshindwa Kuwa Rubani Kwa Sababu ya Filamu", Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Uwoya "Nimeshindwa Kuwa Rubani Kwa Sababu ya Filamu", Ipo Hapa

Staa mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya amesema kuwa filamu zimeharibu mipango yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa mwongozaji wa ndege yaani Rubani.
Uwoya: Nimeshindwa Kuwa Rubani Sababu ya Filamu
Irene alisema hayo weekend hii kupitia kituo cha Radio cha East Africa Radio na kudai kuwa miaka yote aliyokuwa akisoma lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa muongozaji wa ndege Rubani kwani ndiyo kazi aliyokuwa akiipenda na alianza kusoma masomo ambayo aliamini moja kwa moja yangeweza kumfanya kufikia ndoto hizo.
Amesema ndoto yake hiyo iliingia ukakasi baada ya kuanza kufanya filamu za bongo na kujikuta sasa maisha yake yapo kwenye filamu zaidi.

Irene uwoya ambaye alikuwa ni mke wa ndoa wa mchezaji mpira Sulemani Yamin Ndikumana alisema kati ya mwaka 2007 na 2008 ndipo alipoingia katika tasnia ya filamu ambapo anadai kuwa hakuichukulia serious kazi hiyo, sababu tayari alikuwa na mipango ya kusoma na kuja kuwa rubani lakini aliamua kuingia katika tasnia hiyo kufuatia kushawishiwa na baadhi ya watu ambao waliamini kuwa anaweza kuigiza.

"Katikati ya mwaka 2007 na 2008 ndipo niliingia katika tasnia ya filamu nchini tena kwa kushawishiwa na baadhi ya watu, ila mimi nilikuwa nafanya tu sikuwa serious kabisa maana mimi malengo yangu yalikuwa nisome nije kuwa rubani, lakini baada ya kuanza kufanya nikaona watu wananikubali na kupenda kile nikifanyacho na nilipoanza kupata mafanikio nikaona okay kumbe hii ni kazi nikaanza kufanya kazi sasa."

"Nikajikuta sasa maisha yangu yote yameegemea katika filamu na nikaanza kufanya filamu kama maisha mpaka sasa, ingawa kuna kipindi nilikuwa kimya kidogo kutokana na matatizo ya ndoa yangu, maana hakuna kitu kilikuwa kinanitesa kama maneno ya watu, ilifika kipindi nilikuwa siwezi kufanya jambo lolote kwa kuhofia watu, maana nilikuwa naona kama watu wananizungumzia mimi, hivyo kipindi kile kilinirudisha nyuma kidogo, lakini nashukuru Mungu baadaye niliona ni suala la kawaida, maana kuna watu wengi walikuwa katika ndoa na mwisho wa siku ndoa zao zilivunjika na maisha yaliendelea kuanzia hapo ndipo nilipata nguvu na kurudi kuendelea na kazi kama awali, ila kipindi hicho kwa kweli kimenipa taabu sana" Aliongeza Irene Uwoya.

Mbali na hapo Irene alizidi kuweka wazi kuwa kupitia filamu amefanya mambo ya maendeleo mengi sana ikiwepo kuishi maisha yake ayatakayo yeye pasipo kumtegemea mtu yoyote, lakini pia filamu zimeweza kumjengea nyumba ambayo anadai nyumba hiyo inakamilika muda si mrefu tokea sasa.
Amesema hiyo ni mbali na ziara nyingi na mialiko mingi aipatayo nje ya nchi ambayo nayo humjenga na kumpa nafasi zaidi katika kukutana na watu ambao nao wanakuwa na msaada katika kumtengenezea network nzuri ya kazi yake ya sanaa.

Licha ya kuzungumzia mambo mazuri ambayo ndani ya tasnia ya bongo movie lakini Uwoya alisema kuwa kwa sasa tasnia hiyo inaingiliwa na watu ambao wengi wao hawana vipaji wala uwezo wa kuigiza na wanapewa nafasi jambo ambalo linasababisha tasnia hiyo kushuka chini, hivyo anadai kuwa kwa sasa ana mpango wa kukaa na wasanii wenzake.
wakubwa ili waweke mpango wa kuona jinsi gani wanaweza kuzuia watu wasio na vipaji kutoingia katika tasnia hiyo na kuiharibia jina tasnia ya bongo movie ambayo imeweza kubadili maisha ya vijana wengi na kutoa ajira pia kwa vijana wengi.

KWA VIDEOS ZA MASTAA WA BONGO NA VITUKO VYAO FANYA KUBOFYA HAPA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.