PENNY "USISTA DUU UTATUMALIZA MASTAA WA KIKE" SOMA HAPA
Mwanadada superstar Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya wasichana mastaa kujiona masista duu itawamaliza kwa sababu watajikuta uzee unawakabili bila kuwa na ndoa.
Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mastaa wengi wanapenda kujiona ni matawi ya juu na kufikia hatua ya kudharau watu wengine kiasi kwamba hata wenye mapenzi ya dhati kwao hujikuta wakijiweka pembeni hivyo kuwafanya ‘kuchina’ wakati wakitafuta ndoa.
“Unajua kuna vitabia fulani hivi mastaa tunavyo, ya kisista duu ambayo inatufanya tuchine, maana wengi si wanatuogopa wakidhani sisi ni matawi ya juu wakati ni wa kawaida sana,” alisema Penny.
-GPL
Download App Yetu MPYA >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !
No comments
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.