Msanii Mo Music Afunguka Kuhusu Hisia Zake Kwa Lulu, Full Story Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Mo Music Afunguka Kuhusu Hisia Zake Kwa Lulu, Full Story Hapa

Staa wa Bongo Movies, Moshi Katemi  ‘Mo Music’, amesema anatamani kumshirikisha staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika muziki wake kwa kuwa anampenda.
Mo Music: Nampenda Lulu
Msanii huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Basi Nenda’, alisema ametokea kumpenda mrembo huyo kutokana na umahiri wa kazi zake za filamu, maana uwezo wake una tofauti kubwa na waigizaji wengine.
Mo Music aliongeza kwamba huwa ana kawaida ya kutazama filamu za wasanii mbalimbali, lakini za Lulu humvutia zaidi kiasi kwamba anatamani ashiriki kama ‘video queen’ katika muziki wake.
“Ninafuatilia kazi za wasanii mbalimbali, ila kwa Lulu ni tofauti, natamani nimshirikishe katika video za wimbo wangu mpya wa ‘Nitazoea’ kwa kuwa naamini ana mvuto mkubwa,” alimaliza Mo Music.
-bongomovies
ZILE VIDEOS MATATA ZA WAREMBO WAKIKATA VIUNO KWENYE TV YETU, BOFYA HAPA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.