MKE AFUMANIWA NA MTOTO WA MIAKA 16 HUKO MBEYA! MUME ANENA MAZITO ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MKE AFUMANIWA NA MTOTO WA MIAKA 16 HUKO MBEYA! MUME ANENA MAZITO !

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SHANGAA! Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Tumaini Mwashambo (28), mkazi wa Mtaa wa Half Londan, Kata ya Sogea wilayani Momba, Mbeya amejikuta akipokea kipigo kikali kutoka kwa mumewe, Jamsoni Vicent (34) akidai amemfumania na mtoto wa miaka 16 ‘Serengeti boi’.
Tumaini Mwashambo anayedaiwa kupigwa na mumewe. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Jamsoni alisema ni mara ya pili kumfumania mke wake na huyo mtoto ambapo alisema anaamini ni sawa na kumbaka.
“Mara ya kwanza niliwakuta wanaangalia mkanda wa ngono huku wakiwa peke yao, yeye na mtoto huyo kwenye nyumba yangu. Nilimuonya Tumaini kuwa tabia hiyo si nzuri lakini hakutaka kunisikiliza,” alidai mwanaume huyo.

Aliendelea kudai kuwa, mara ya pili alimkuta tena mkewe huyo akiwa amempakata mtoto huyo huku wakilishana mayai, pia mke akiwa amevaa kanga moja.

“Nilishangaa sana mke wangu kuwa na tabia kama hiyo ya ubakaji lakini niliishia kumuonya tu. Kweli za mwizi ni arobaini kwani nilikuja kumkamata mke wangu akiwa na mtoto huyo chumbani lakini kutokana na mimi kuwa na hasira nilianza kumpa kichapo mke wangu kwa sababu naamini ndiye aliyemtongoza mtoto huyo,” alisema.

Aliongeza: “Nilimpiga mke wangu hadi nikamjeruhi sehemu za kichwani lakini cha ajabu, aliondoka na kwenda kulala nyumbani kwa mama wa mtoto huyo. Mimi nilijua labda anataka kuolewa naye.
“Ndugu zangu wameniambia mke wangu siyo yeye, ana pepo anamsumbua ndiyo maana amekuwa na tabia ya kuwatamani watoto wadogo.”

Baadaye Uwazi lilimsaka mwanamke huyo ambaye naye alijieleza:
“Ni kweli mimi huwa ninashinda na mtoto huyo na muda mwingi nakuwa kwao huku nikiwa nimeacha nyumba yangu. Lakini siyo kwamba natembea naye, huyo mtoto hawezi kunipa kitu chochote, hata mahitaji yangu. Kwanza hata mimi jamii itanichukuliaje kama siyo mbakaji tu, hayo ni maneno ya watu tu. Jamsoni si kwamba alinifumania, alimwita yule mtoto nyumbani alipoingia akamwambia avue nguo, sijui alitaka kufanyaje.”

Pia mwanamke huyo alikiri kuwa, amemkosea sana mumewe hivyo akaomba amsamehe na warudiane ili waendelee kulea watoto wao.
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa aliyetajwa kwa jina moja la Juma na mjumbe wa eneo hilo, walipinga vitendo hivyo vichafu katika mtaa wao na kusema endapo tukio la mwanamke huyo litajirudia watashitakiwa na serikali.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.