Exclusive: Shamsa Ford Afunguka Kuhusu Nay Wa Mitego, Kasemaje ? Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Exclusive: Shamsa Ford Afunguka Kuhusu Nay Wa Mitego, Kasemaje ? Ipo Hapa

Muigizaji wa filamu ya ‘Chausiku’, Shamsa Ford amemmwagia sifa rapper Nay wa Mitego kwa kudai hakuwahi kujua kama ni mkarimu huku akidai kuwa anafaa kuwa mume!
Nayy
Shamsa ambaye aliachana na mume wake tangu October mwaka jana, ameiambia Bongo5 kuwa aliombwa na Nay ashirikishwe katika filamu yake.
“Sisi ni washkaji sema Nay ana kazi yake ya filamu ndio akaona mimi ndo nafaa, Hakuna kitu chochote zaidi ya kazi,” amesema Shamsa.
“Kabla ya kupata nafasi ya kuongea na Nay nilikuwa namuona ni mtu fulani mgomvi mgomvi, in short nilikuwa simpendagi! Kama unakumbuka aliwahi kutuponda Bongo Movie na mimi kuna siku nilihojiwa na kituo kimoja nikamponda sana! Lakini nimekuja kukutana na Nay nimegundua ni mtu tofauti sana. Sasa hivi mimi namzungumzia Emmanuel is man ambaye kila mtu au kila mwanamke anaweza akamhitaji kuwa naye! Ana huruma ana upendo, he is a good man, kama nilivyosema mwanamke yoyote atapenda kuwa naye. Kwahiyo ni husband material,” aliongeza Shamsa.

Kwa upande mwingine, Shamsa amewataka mashabiki wa kazi zake kutambua kuwa yeye ni mtu mzima na ana maamuzi ya kufanya kile anachokipenda ili mradi asiharibu kazi.
“Mashabiki wangu wajue Shamsa mimi najielewa najitambua ni mkubwa na ninajua zuri na baya,” amesisitiza muigizaji huyo. “Wasinihukumu kwa ambacho wanakiona au wanachokisikia, wanisubiri mimi kama mimi Shamsa na hayo wanayoyasikia hayawezi kuniharibia mimi kazi zangu au kuachana mimi na mume wangu ndo nitashuka kisanii, hapana! Wasihukumu hivyo, mimi nipo makini na kazi zangu.”

-bongo5
JIONEE VIDEOS ZA VITUKO, INTERVIEW, SHOW NA HABARI ZA MASTAA WA BONGO KUPITIA BS Tv, BOFYA HAPA Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.