EXCLUSIVE; IMEVUJA KUWA ROSE NDAUKA NA MANECKY WAPO KWENYE PENZI ZITO ! IPO HAPA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

EXCLUSIVE; IMEVUJA KUWA ROSE NDAUKA NA MANECKY WAPO KWENYE PENZI ZITO ! IPO HAPA

Bet Sasa
IMEVUJA! Baada ya uhusiano wake na Mbongo Fleva, Malick Bandawe kuvunjika, staa wa sinema Bongo, Rose Ndauka kwa sasa anadaiwa kuzama kwenye penzi zito la Prodyuza wa Bongo Fleva, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.
Msanii nyota wa sinema za Bongo Movie, Rose Ndauka.
Kwa mujibu wa chanzo, kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa wakionekana sambamba kama kumbikumbi hasa nyakati za usiku katika maeneo tofauti ikiwemo studio ambayo Manecky anafanyia kazi zake na sehemu nyingine. “Rose na Manecky ni wapenzi kwani muda mwingi wako pamoja, wanaongozana kama kumbikumbi hasa usiku. Huwa tunawaona wanakuja maeneo ya hapa Afrika Sana wanakwenda kununua chakula cha jioni huku Manecky akijinadi kuwa ameamua kuwa na Rose kwa kuwa mke wake halali hivi sasa ni mjamzito,” kilisema chanzo hicho.
Prodyuza wa Bongo Fleva, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.
Mara baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao ili kuweza kujibu tuhuma hizo ambapo Manecky alipopatikana alikanusha na kudai ukaribu wao unaletwa na kazi. “Ukaribu wangu mimi na Rose ni kazi tu kwani kuna ‘project’ tunaifanya nadhani mwenyewe Rose ndiyo anaweza kuweka wazi hilo, kingine Rose anafanya kazi na mdogo wangu kwenye gazeti la Rozzie la mtandaoni,” alisema Manecky.
Alipoulizwa kama ameamua kutembea na Rose kwa sababu mkewe ni mjamzito, Manecky alizidi kusisitiza kuwa si kweli. “Hamna kitu kama hicho jamani.” Ili kupata upande wa pili, mwanahabari wetu alimvutia waya Rose ili kujua anazungumziaje tuhuma hizo likiwemo suala la kuonekana na Manecky mara kwa mara, naye aliruka viunzi:
“Hakuna kitu kama hicho jamani, kwani mimi nachaguliwa mtu wa kukaa naye? Acheni kusikiliza maneneo ya watu halafu Manecky ana mke ambaye ni mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote,” alisema Rose. Rose na Malick kabla ya kumwagana miezi michache iliyopita, walidumu kwenye uhusiano kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.