Davido apost picha akiwa na Diamond studio na kuandika ujumbe uliotuacha njia panda! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Davido apost picha akiwa na Diamond studio na kuandika ujumbe uliotuacha njia panda!

Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother Africa.

11057685_371329423067689_4700138123020625793_n
Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi

Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram.
Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”
Davido

Picha hiyo imevutia comments nyingi japo asilimia kubwa ni za wakenya wanaomnyeshea mvua ya matusi! Yes, Wakenya hawataki kumsikia tena Davido!
Hakuna shaka kuwa staa huyo wa Nigeria ana picha nyingi ambazo angeweka kuambatanisha na ujumbe huo. Hivyo, uchaguzi wa picha akiwa na Diamond unaweza ukawa na dhumuni maalum!
-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.