CELEBRITIES GOSSIP: WEMA AFUNGUKA ASEMA ''SINA KINYONGO NA DIAMOND ILA YEYE ANACHO KWANGU! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

CELEBRITIES GOSSIP: WEMA AFUNGUKA ASEMA ''SINA KINYONGO NA DIAMOND ILA YEYE ANACHO KWANGU!

Wema Sepetu amesema hana kinyongo na ex wake Diamond bali hitmaker huyo wa ‘Nasema Nawe’ ndiye bado ameendelea kuwa na kinyongo naye.
wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg
Akizungumza kwenye kipindi cha Ubaoni cha EFM leo, Wema alisema kuna siku alimtumia ujumbe wa simu Diamond kumpa pole kwa kumuuguza mama yake lakini alimchunia.
“Tumeshaachana kwanini tuwekeane grudges,?”alihoji Wema kwenye kipindi hicho. “Tulikuwa pamoja lakini tumeachana kwanini tuwekeane bif, kinyongo? Mimi leo na kesho nikutana na mtu kama Jumbe siwezi kumpita nikasema nisimsalimie! Nikutana na mtu kama Chaz Baba, Chaz Baba mara ya mwisho juzi kaja nyumbani kaja kaniona alikuwa kaniletea kambwa tuongea kishkaji! Kwahiyo kama ulikuwa na mtu halafu mkaachana hamtakiwi kuwekeana kinyongo,” alisisitiza.
“Mimi siwezi kuwa na kinyongo na Diamond hata siku moja lakini imekuwa iko tofauti kwa sababu mwenzangu hayuko hivyo anataka ile no! No! sijui ni kwa nini lakini labda kila mmoja ana jinsi anavyofikiri.”
“Sijawai kumpigia simu ila nilishawakumtext, nilisikia kwamba mama yake anaumwa baada ya kusikia mama yake anaumwa nilim-text kama pole kwa sababu sina kinyongo naYe nikampa pole lakini kama nilivyoowambia mwenzangu yupo tofauti, nilifanya kibinadamu yule mama mimi hajanikosea.”
KWA ZILE VIDEOS ZA MASTAA WA BONGO NA VITUKO VYAO, BOFYA HAPA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.