UNAIKUMBUKA HII ? WANAUME WAVAA SKETI KU- SUPPORT MAANDAMANO YA WANAWAKE. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

UNAIKUMBUKA HII ? WANAUME WAVAA SKETI KU- SUPPORT MAANDAMANO YA WANAWAKE.

Kuna namna mbalimbali ya kusupport harakati, unaweza ukabeba bango lako mwenyewe, au siku hizi teknolojia, unaweza ukaingia zako tu Twitter halafu unaweka hashtag, basi unakuwa umetoa support yako ya nguvu.Hawa jamaa wa Uturuki wameona isiwe tabu, wameingia zao na wenyewe mtaani wakiwa wamevaa zao sketi za wanawake ili tu ku show support yao ya nguvu kwa wanawake ambao walikuwa wakiandamana kulaani mauaji ya mwanamke mmoja Ozgecan Aslan ambaye aliuawa na mwanaume aliyetaka kumbaka.

Wanawake wakaingia mtaani kudai haki zao kwa kuwa kitendo hicho kilionyesha ukatili na unyanyasaji wa wanawake kwa hali ya juu, wanaume wanaosupport nao wakaongeza nguvu kwa kuvaa sketi pia na kuandamana.
Wababa na sketi zao kwenye maandamano.

Hawa huenda majukumu yaliwabana wakashindwa kuingia mtaani kuandamana, basi wakatupia PICHAZ na sketi zao mitandaoni.

Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.