Umepata Stori Hii Ya Maiti Kuzinduka wakati Wa maandalizi ya mazishi ? Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Umepata Stori Hii Ya Maiti Kuzinduka wakati Wa maandalizi ya mazishi ? Ipo Hapa

Bet Sasa
Toetag
Zimesikika story za watu kuzinduka wakiwa mochwari.. Huyu kapata fahamu kwenye mazingira ambayo yalisababisha mtu ambaye ana jukumu kufanya uangalizi wa maiti nae kupata matatizo mengine.
Mwanamke mmoja Ujerumani alipata fahamu akiwa ndani ya jeneza chumba cha kuhifadhia maiti, akaanza kujiburuza kutoka ndani ya jeneza, jamaa ambaye anasimamia chumba hicho cha kuhifadhi maiti akazimia baada ya kumuona.. alipozinduka mwanamke huyo akamuuliza; “kwani hapa niko wapi?”, jamaa huyo akapiga simu kuomba msaada wa ambulance.
Ambulance ilifika na kumchukua mwanamke huyo kumpeleka Hospitali ambapo siku ya pili yake akafariki tena wakati akipata matibabu.
Polisi wanachunguza juu ya ishu ya kilichofanya mwanamke huyo kuonekana amefariki kwa mara ya kwanza ambapo ndugu wa marehemu huyo walimkuta akiwa hana fahamu kitandani kwake.
-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.