Lulu Afunguka "Shule Inanizuia Kujirusha " - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Afunguka "Shule Inanizuia Kujirusha "

Staa  mrembo kutoka Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekiri kuwa ubize wake katika masomo umemzuia kwa kiasi kikubwa kupata muda wa kufikiria mambo ya kijinga na hata kujirusha.
Shule Yamzuia Lulu Kujirusha
Akiongea na paparazi wa GPL, Lulu alisema mtu akisimamia kwenye masomo hawezi kuwa na mawazo mabovu kama ya kwenda kujirusha au kupata kilevi badala yake unajikuta ukifikiria masomo na mitihani tu.
“Jamani kama mimi sasa hivi sina hata ninachokiwaza zaidi ya masomo yangu na mitihani ninayokutana nayo yaani hata muda wa kusema utaenda Club, hakuna nafasi kabisa katika kichwa, hivyo nimeamini kuwa ukiwa bize na masomo akili za ajabu hazipo kabisa,” alisema Lulu.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.