Lil Wayne kuhusu album mpya na mpenzi wake mpya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lil Wayne kuhusu album mpya na mpenzi wake mpya.

christinamilianlilwayne
Rapa Lil Wayne amesema yupo tayari kutoa album yake mpya ya “Free Weezy Album” mwezi wa nne mwaka huu 2015.
Lil Wayne anasema album itatoka kama solo projet yake mwenyewe ikiwa ni ya pili baada ya Sorry 4 Tha Wait iliyotoka January baada yakushindwa kutoa Tha Carter 5.
Wayne ambaye ni Bosi wa kundi la Young Money, amemuweka wazi mpenzi wake mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo analoliongoza. Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter, aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.