Exclusive; Ugumba Wamtesa Wema, Adondosha Chozi Mara kwa Mara ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Exclusive; Ugumba Wamtesa Wema, Adondosha Chozi Mara kwa Mara !

Tatizo la kutoshika mimba (infertility) au kushindwa kupata mimba (conceive) limekuwa likimtesa staa wa Bongo Movies, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na limehusishwa na ugumba.
Ugumba Wamtesa Wema, Adondosha Chozi Mara kwa Mara! 1
Akizungumza na gazeti la Amani juu ya ishu hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Wema alisema suala la kutopata mtoto limekuwa likimkosesha amani katika maisha yake ya ukubwani.
Alisema kwamba, amekuwa akishinda akilia kila anapokutana na shosti wake wa sasa, Aunt Ezekiel ambaye ni mjamzito.Wema alitiririka kwamba, kila wakati amekuwa akimwambia Aunt kuwa na yeye anatamani kupata mimba lakini Mungu hajamjalia. Kwa kusema hivyo, huwa wanajikuta wakikumbatiana na kuangua vilio wote kwa pamoja.Ugumba Wamtesa Wema, Adondosha Chozi Mara kwa Mara!
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Staa huyo wa Bongo Movies ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, mwanadada huyo anaona umri umeenda sana kwani tayari ana miaka 26 sasa.
“Unajua Wema alishajaribu kupata mtoto mara kadhaa ikashindikana na umri nao unakwenda hivyo lazima akose amani. Hebu fikiria aliwahi kuwa na Kanumba (marehemu Steven), Jumbe (Yusuf), Chaz Baba (Charles Mbwana) na Diamond (Nasibu Abdul) lakini kote huko alitoka kapa.
“Mbaya zaidi ni maneno yanayosemwa na watu yanamuumiza sana, wanasema ni mgumba kama ilivyokuwa kwa Jide (mwanamuziki Judith Wambura ‘Jaydee’).“Kwa kweli hali hiyo inamtesa sana ila watu hawajui bora wakafunga vinywa vyao na kuacha kuandika kwenye mitandao ya kijamii,” alifunguka mtu huyo wa karibu.
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kwamba, Wema amekuwa akilia kila anapowaona ma-Miss Tanzania wenzake wakiwa na watoto wao.
Ilisemekana kwamba warembo ambao wanamliza ni Wema Nancy Sumary (Miss Tanzania 2005), Faraja Kota (2004), Hoyce Temu (1999), Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-lynn’ (2000) na Miriam Gerald (2009).
Ilisemekana kwamba wengine aliokuwa nao kwenye shindano hilo mwaka 2006 ambao wana watoto ni Lisa Jensen, Aunt Ezekiel na wengine ambao kwa pamoja wamekuwa wakimfanya naye atamani kupata mtoto.
Chanzo:GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.