Kama ulikuwa hujui basi naku habarisha, mastaa ambao wameshibana kwa sasa, namzunguzia wema sepetu pamoja na aunty Ezekiel, hapo awali waliwahi kuingia kwenye bifu zito kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la aliyekuwa mcheza filamu maarufu nchini, marehemu kanumba. Bifu hilo lilifikia pabaya ambapo mastaa hao walirushiana maneno makali kwenye mitandao kila mmoja akimshtumu mwenzie kumuibia bwana ake, bifu hilo lilidumu kwa mda mrefu, lakini sasa ivi mastaa hao wameshibana na kuishi kama ndugu, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.

Unakumbuka kipindi kile kwenye Interview ya zamaradi mketema alipowahoji irene uwoya na wema sepetu kuhusu bifu lao na jackline wolper? Bifu lilikuwa zito, ambapo chanzo kinadaiwa kuwa ni mwanaume, warembo hao walinuniana na kutupiana maneno machafu mitandaoni. Ivi sasa mastaa hao wanaishi kwa amani na maisha yanaendelea.