Baada ya Kusambaa kwa Stori ya Kutoka na Aliekuwa Bwana wa Wolper , Wastara Amesema Haya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Kusambaa kwa Stori ya Kutoka na Aliekuwa Bwana wa Wolper , Wastara Amesema Haya

Baada ya Kusambaa kwa  Stori ya Kutoka na Aliekuwa Bwana wa Wolper , Wastara Amesema Haya
Kupitia ukurasa wake wa ‘facebook’ Wastara amendika maneno haya;
“Kalamu ya muandishi imegeuka kuwa fimbo ya wanyonge tofauti na miaka ya nyuma,waandishi wanakula mishahara mara mbili wa kituo anachofanyia kazi na wa mtu anaempa habari,hivyo kuandika anachoambiwa sio anachokiona
Pesa inatumika kupotosha ukweli na ukweli ndio uongo waleo,nimeamini maneno yangekuwa sumu ningeshakufa zamani sana lakini kwakua mdomo nyumba ya maneno bado niko hai
Tupendane tushikamane na tuishi kwa usawa usipende kuonea unachoambiwa ongea unachokijua,sio pesa ikufanye kuharibu image nzima ya mtu kwanza kwa pesa gani?
Allah ndio amenitengeneza na ndio atakaenichukua akiamu na ndio mwenye uwezo wa kunishusha na kunipandisha lakini sio wewe tuliokutana duniani”.- wastara alimaliza.
Hivi juzi kati Watara alidaiwa kutoka na alikuwa bwana wa Jaqline Wolper anaefahamika kwa jina la  Mark Edi ambae ni mfanya biashara wa mavazi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.