Huu Ndio Wimbo Wa Kwanza Kumtambulisha Aslay Kwenye Muziki 'Nakusemea' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huu Ndio Wimbo Wa Kwanza Kumtambulisha Aslay Kwenye Muziki 'Nakusemea'

Mwonekano wa Enzi hizo wa mwanamuziki Aslay kabla ya kuwa Staa.
Kutoka kuitwa Dogo Aslay mpaka mwanamuziki mkali bongo Aslay amekuwa msanii asiyekata tamaa jambo ambalo limemfanya sasa hivi kuwa gumzo na kujizolea mafanikio mengi. Kama haukuwa unafahamu wimbo 'Nakusemea' ndio uliompa upenyo wa kuingia kwenye game ya muziki wa Tanzania kabla ya kuja kujiunga na kufanya vizuri akiwa kwenye kundi la Yamoto Band.

Tazama video ya wimbo huo hapa chini:
Aslay kwa sasa anafanya mziki wake kama msanii wa kujitegemea baada ya kundi alilokuwepo la Yamoto Band kuvunjika. Hivi karibuni aliachia ngoma kibao ikiwemo 'Natamba, Hauna, Likizo, Nibebe, Kwa Raha huku akiwa kati ya wasanii wanaokubalika sana na ambae ukimweka kwenye wimbo wako ni lazima afanye maajabu na wimbo utafanya vizuri.
Huu ni mwonekano wa sasa wa Aslay baada ya kuwa staa mkubwa Tanzania

Huyo ndiye Aslay kwa ufupi, Nafikiri kwa picha hizi umeweza kupata hamasa na kufahamu alipotoka msanii huyu anayesumbua kwenye spika za redio, simu na Tv kibao Tanzania na Afrika Mashariki. Kama wewe ni shabiki wa kweli wa Aslay na ungependa kufuatilia habari na nyimbo zake za nyuma na mpya basi  >Bofya Hapa< 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.