HAWA NDIYO WASANII 6 WA BONGO NA MAREKANI WANAOENDANA UMRI SAWA NA DIAMOND PLATNUMZ MPAKA SASA...!! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

HAWA NDIYO WASANII 6 WA BONGO NA MAREKANI WANAOENDANA UMRI SAWA NA DIAMOND PLATNUMZ MPAKA SASA...!!


Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam.Kwa mwaka huu diamond anategea kufikisha robo karne kwa kutimiza miaka 25. Akiwa huu ni mwaka wa 6 ndani ya game ungeweza kufikiria jamaa ameshachoka lakini chakujua ni kwamba umri wake bado unaruhusu.tovuti hii inakuletea list ya celebrities ambao wanamiaka sawa na diamond platnumz.
Ben Pol
Benard Michael Paul Mnyang’anga au unaweza kumuita ben pol alizaliwa september 8, mwaka 1989. Kwasasa ben pol ndiyo mfalme wa muziki wa Rnb hapa Tanzania na ni mtu ambaye anaweza kufanya anayoyafanya diamond kutokana na yeye kuchelewa kidogo kufika kwenye game.

Chris Brown
Christopher Maurice Brown alizaliwa  May 5, 1989 . Huyu naye ni mkali mwingine wa RnB kutoka Marekani ambaye naye alianza muziki akiwa na umri mdogo sana yaani miaka 16.

Rose Ndauka
Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10) mwaka 1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa. ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana.Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia rose ni mwandishi na mwongozaji wa Filamu.

Jordin Sparks & Jason Derulo
Jordin Sparks alizaliwa December 22 mwaka 1989. Mkali huyu wa miondoko ya RnB  alitoka baada ya kuibuka mshindi wa msimu wa sita wa mashindano ya kusaka vipaji ya American idol .Jason Derulo mkali wa “talk dirty” naye alizaliwa tarehe 21 september mwaka 1989. Jason Derulo na Jordin Sparks kwasasa ni couples and how sweet is it kua na couples wenye umri mmoja.

Emmanuel Mkono (Nahreel)
Nahreel alizaliwa December 12 mwaka 1989. Nahreel ni mmoja wa producer anayesumbua sana kwasasa na amefanya ngoma kama nje ya box ya weusi na come over ya vanessa mdee. pia jamaa ni mmoja ya waimbaji wa kundi la weusi.

Vibe Magazine

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.