Mr. Nice Amchana Dudu Baya, Adai Hana Mahali Pa Kuishi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mr. Nice Amchana Dudu Baya, Adai Hana Mahali Pa Kuishi

Msanii Mr Nice ambaye kwa sasa ameachia kazi yake mpya ya Yaya, amejibu tuhuma za msanii mwenzake Dubu Baya aliposema kwamba maisha yamemshinda na kukimbilia Kenya, na kumjibu kuwa Dudu Baya ni msanii asiyejielewa, ndio maana hana mahali pa kuishi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teleivison, Mr.Nice amesema ni wakati sasa Dudu Baya akomae na game kama anavyofanya yeye, kwani muda wa malumbano na kuchafuana hautamsaidia chochote, na hastahili kufanya hayo kwakuwa umri umeshamuacha.

Mr. Nice ameendelea kwa kusema kwamba Dudu Baya ni mlevi na anaishi maisha ya kuigiza, hivyo kabla hajaanza kumuongelea vibaya ni vyema akaanza kujilinganisha naye kama wanafanana kimaisha.

EATV
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.