Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Mwalimu Ajiua kwa Sumu Akiwa Gesti, Aacha Ujumbe Mzito


SUMBAWANGA. Mwalimu, Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kwamba mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.

Kyando amesema chanzo cha kifo cha mwalimu huyo bado hakijafahamika lakini aliacha ujumbe mfupi wa maneno.
“Kama anadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wake, lakini asilaumiwe chochote juu ya kifo chake,” amesema Kamanda Kyando wakati akinukuu ujumbe huo wa marehemu.
Kamanda Kyando pia amesema uchunguzi wa kitabibu umebainisha kuwa mwalimu huyo alijiua kwa kunywa sumu.

-GPL
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.