Advert

Breaking News

Hii hapa Taarifa kuhusu rufaa ya Simba kwa mchezaji wa Kagera Sugar

KIKAO cha kamati ya masaa 72 kilichokaa Ijumaa April 7, 2017 kwenye ukumbi wa ofisi za shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujadili rufaa mbalimbali ambazo zilitokea kwenye ligi kuu na michezo ya Play off ya SDL kimemalizika Salama.

Kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu ni rufaa ya Simba Kwa Bodi ya ligi wakidai wapewe pointi za mchezo dhidi ya Kagera sugar uliochezwa Jumapili iliyopita na Simba kufungwa Kwa magoli 2-1. Simba walimkatia rufaa mchezaji Mohamed Fakhi wa kagera Sugar wakidai alicheza akiwa na kadi tatu za njano na hivyo Kagera kukiuka taratibu na kanuni za ligi kuu ya Vodacom Tanzania.

Kamati ya Masaa 72 imetoa ufafanuzi kuwa Maamuzi ya rufaa ya Simba dhidi ya Mohamed Fakhi yatatolewa Alhamisi ya wiki Ijayo.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.