Advert

Breaking News

Producer Mpya wa Free Nation Adai Album ya Nay wa Mitego Ipo Tayari.

Inawezekana mwaka huu, hitmaker wa Sijiwezi, Nay Wa Mitego akafungua ukurasa mwingine wa muziki wake kwa kudondosha album yake. Producer mpya wa studio ya Free Nation ambayo Nay anaimiliki, Ossam,ameiambia Dizzim Online kuwa album hiyo ipo tayari na kinachosubiriwa ni kukamilishwa kwa mipango ya management.

Ossam amechukua nafasi ya Mr T Touch aliyekuwa kwenye studio hiyo kabla ya kuondoka na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe.Hivi karibuni Nay amekuwa akionesha picha zinazoonesha muonekano tofauti wa studio zake ambazo amekuwa akitumia muda mwingi kurekodi nyimbo mpya.

Kwenye picha moja aliyoweka Instagram, Nay ameandika, “Hii kazi nimeichagua mwenyewe acha nipambane. Wao wana Kesha kwenye Starehe, wana Kesha Club sisi tuna Kesha Kazini.!! Tutakutana kwenye Maendeleo🔥✊🏿. Utavuna Ulicho Panda✊🏿.”
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.