Advert

Breaking News

Mc Pilipili Aweka Wazi Mpango wa Kuoa.

Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias aka MC Pilipili amedai anasumbuliwa na familia yake kuhusu suala la kuoa.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, MC pilipili amesema kwa sasa anajipanga kuingia kwenye maisha ya ndoa baada ya kumpata mtu sahihi ambaye anaweza kumuoa.

“Hivi karibuni Mama yangu alikuwa anahojiwa pamoja na wadogo zangu wote wakaulizwa ni kitu gani kinawakera kutoka kwa MC pilipili wakasema hataki kuoa,” alisema MC Pilipili. “Lakini mimi sisemi nataka kuoa kwa sababu ya kushinikizwa, lakini mambo yakikaa sawa nitaoa kwa sababu nina msichana mzuri sana,”

Pia mchekeshaji huyo amesema anaendelea na ziara yake ya kuandaa matamasha ya kuchekesha mikoani ambapo safari hii anajipanga kufanya tamasha kubwa Dodoma.


-Bongo5
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.