Advert

Breaking News

Sergio Agguero Kuikosa Manchester Derby


Na Halidi Abdulrahman


Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero rasmi ataukosa mchezo wa Manchester Derby baada ya kufungiwa michezo mitatu na Chama cha Soka nchini England, FA kufuatia kitendo kisicho cha kiungwana.

Aguero alimpiga kiwiko mlinzi wa West Ham, Winston Reid kwenye mchezo wa wiki iliyopita ambapo Manchester City iliibuka na ushindi.

Manchester City itamenyana na Manchester United katika mchezo wa Manchester Derby wiki ijayo huku akitarajiwa kuikosa michezo mingine miwili ukiwemo dhidi ya Bournemouth.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.