Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Rais Magufuli Ananikubali Mpaka Basi - Christian Bella

Christian Bella ameungana na Mrisho Mpoto kwenye orodha ya wasanii waliopo kwenye playlist ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Beatz cha Star TV, Bella alisema Rais Magufuli anamkubali hadi basi! Amesema kwake kukubalika na Rais wa nchi ni heshima kubwa na kumbukumbu atakayoitunza milele.

Bella amedai ni muhimu kwakuwa hajawahi kuwambia kitu kama hicho na rais yeyote tangu aanze kufanya muziki. “Ni kitu kikubwa sana kwangu na sikutegemea,” alisema.

“Sijawahi kuambiwa na na rais yeyote, rais wangu ni Magufuli nampenda sana,” alisema Bella.

Hivi karibuni Mrisho Mpoto naye alionesha furaha yake baada ya Dkt Magufuli kumwambia kuwa anaupenda wimbo wake ‘Sizonje.’ Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.