Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Professor Jay Aeleza Anavyoziheshimu Harakati za Joh Makini.

Msanii mkongwe wa hip hop nchini,Professor Jay amesema kuwa anaheshimu sana harakati ambazo msanii Joh Makini anazifanya kuupeleka muziki wa hip hop ya bongo kimataifa.

Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Jay amempongeza Joh Makini kwa kuchaguliwa kuingia kwenye tuzo za Afrimma na kuomba watanzania wamsapoti.

“Nina respect sana struggle za joh Makini,jinsi anavyotafuta tundu la kupenya kimataifa.Na pale haendi peke yake ni Tanzania inaenda pale.Napoona anafanya kolabo na A.K.A ,Chidnma, mimi nafurahi,na yeye kuwa nominated kwenye tuzo za Afrimma ina maana muziki wake umeshaanza kupata soko kimataifa inabidi tuungane kumsapoti.“alifunguka mkongwe huyo wa Hip Hop anayetamba na wimbo wake wa kazi kazi ambao upo kwenye mahadhi ya singeli.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.