Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Diamond Platnumz: 'Zari Atajifungua Mwezi Disemba, Mtoto Wa Kiume'

Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.

“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”

Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”

Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.