Advert

Breaking News

Birthday ya Mwisho ya Obama Akiwa White House Ni Noma.

Sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rais wa Marekani anayeondoka madarakani, Barack Obama iliyofanyika kwenye ikulu ya White House, ilikuwa noma kwa mujibu wa mgeni aliyehudhuria na kuongea na mtandao wa Page Six.
Hiyo ilikuwa birthday yake ya mwisho akiwa ikulu hiyo ambapo ametimiza miaka 55. Kulikuwepo na wageni wazito wakiwemo George Lucas, Nick Jonas, Ellen DeGeneres, Magic Johnson na Sarah Jessica Parker.

Stevie Wonder na Usher walitumbuiza kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa na mkewe, Michelle Obama. Pia kulikuwepo na mastaa kama mchezaji wa kikapu, Chris Paul na wasanii wa hip-hop Common, Kendrick Lamar na Timbaland.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.