Kuketi Muda Mrefu Kunaweza Kukusababishia Magonjwa Haya.

TATIZO la kuketi kwa muda mrefu ni mojawapo ya matatizo yanayoongezeka kwa kasi hapa nchini. Mabad...


TATIZO la kuketi kwa muda mrefu ni mojawapo ya matatizo yanayoongezeka kwa kasi hapa nchini.

Mabadiliko ya kiuchumi kwa kiasi kikubwa yamechangia kusababisha tatizo hili. Mpaka hapa wengi wenu mnaweza mkawa mnajiuliza–ni nini haswa sababu ya kusema kuketi kwa muda mrefu ni tatizo, wakati wengi wetu tukidhani ni starehe.

Kuketi kwa muda unaozidi saa nane kwa siku kunaweza kukusababisha kifo, ambacho katika hali ya kawaida kinazuilika. Utafiti mkubwa uliofanyika kwa zaidi ya miaka 12 huko nchini Marekani umebainisha hayo.

Katika utafiti huu wataalamu waliwafuatilia wanawake takribani 100,000; kwa muda wa miaka isiyopungua 12. Utafiti huu ambao ulianza mwaka 1993 ulihusisha wanawake wenye umri kati ya miaka 50-79, na uliendelea mpaka mwaka 2010.

Wanawake hawa walirekodi muda waliokuwa wakiutumia kuketi, na watafiti waliendelea kuwafuatilia wanawake hao mara kwa mara.

Kutokana na muda waliokuwa wakiutumia kuketi, wanawake hawa waligawanywa katika makundi manne.

Wale waliokuwa wakitumia chini ya saa nne kuketi, waliokuwa wakitumia kati ya saa nne mpaka nane kuketi, walikuwa wakiketi kwa muda wa saa kati ya nane na 11, kundi la mwisho ilikuwa ni wale waliotumia zaidi ya saa 11 kwa siku, wakiwa wameketi.

Baada ya kuwafuatilia wanawake hawa kwa takribani miaka 12, ilionekana kwamba, ukilinganisha na wale waliotumia saa chache kuketi, asilimia kubwa ya wanawake waliotumia muda mwingi zaidi kuketi walipoteza maisha katika kipindi hicho cha miaka 12.

Vifo hivyo vilivyowakuta wanawake hawa vilitokana na sababu tofauti tofauti vingi vikiwa vinatokana na mojawapo ya magonjwa sugu kama vile kisukari, magonjwa ya moyo na aina fulani ya saratani.

Cha kustaajabisha zaidi ni ukweli kwamba, namba ya waliopoteza maisha katika wale waliokuwa wakitumia zaidi ya saa 11 kuketi, ilikuwa kubwa kuzidi wale waliokuwa wakitumia kati ya saa nane na 11.

Namba ya waliopoteza maisha katika hawa waliokuwa wakitumia kati ya saa 8-11 kuketi ilikuwa kubwa kuliko ile ya wale waliokuwa wakiketi kwa saa 4-8.

Na kiasi kidogo mno cha wale waliokuwa wakitumia chini ya saa nne kuketi, walipoteza maisha. Hii inaonyesha kwamba kadri muda au dosi ya kuketi inavyoongezeka, hivyo hivyo hatari ya kupoteza maisha kutokana na magonjwa sugu inaongezeka.

Utafiti huu ni mmoja kati ya tafiti nyingi zilizofanyika sehemu mbalimbali za dunia, na kuonyesha kwamba kuketi kwa muda mrefu kunatuongezea uwezekano wa kupata magonjwa sugu hivyo kukuweka katika hatari ya kufikwa na mauti inayoweza kusababishwa na magonjwa hayo. Kuketi kwa muda mrefu kunachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha maumivu sugu ya mgongo na hata magoti.

Upo ushahidi wa kiutafiti unaoonyesha watu kupata ulemavu wa kudumu kwa ajili ya kuketi kwa muda mrefu.

Kuna tafiti zilizoonyesha kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili wanaotumia kompyuta mara kwa mara ana matatizo sugu ya misuli na viungo yanayotokana na kuketi kwa muda mrefu.

Ziko hata tafiti zinazoonyesha kwamba, hata kama unatimiza kiwango cha mazoezi kinachoshauriwa katika kujikinga na magonjwa, kutumia zaidi ya saa nane ndani ya siku moja kuketi ni hatari.

Ikumbukwe kwamba, tunapozungumzia kuketi kwa saa nane, haimaanishi kuketi kwa saa nane mfululizo, bali ukijumlisha saa zote unazokuwa umeketi hususani katika saa 12 ya mchana, muda huo ufike saa nane au zaidi.

Kwa kawaida tunaketi tukiwa katika magari, maofisini, na tunapokuwa nyumbani tukiangalia TV.

Wanasayansi bado wanafanya tafiti ili kulifahamu kwa undani tatizo hili. Hata hivyo, ni vizuri kufahamu kwamba kuketi kwa muda mrefu, hususan zaidi ya saa nane kwa siku, kiafya si kitu kizuri.

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao shughuli zao za kila siku zinawalazimu kuketi kwa muda mrefu, unaweza kabisa ukawa unajiuliza unafanya nini kuepukana na tatizo hili.

Hizi hapa njia mbili

zilizofanyiwa tafiti na kuhakikiwa katika kupunguza athari za kiafya zinazoweza kusababishwa na kuketi muda mrefu:

Mapumziko mafupi ya mara kwa mara

Kwa mtu mwenye kazi inayomlazimu kuketi muda mrefu, tafiti zimeonyesha kwamba kupumzika na kusimama au kutembea angalau kila baada ya saa moja kunasaidia kupunguza makali ya athari za kiafya zinazoweza kusababishwa na kuketi kwa muda mrefu.

Jiwekee mapumziko ya takribani dakika tano mpaka 15, ambako unautumia muda huo kusimama, kutembea au kujinyoosha.

Kubadilisha mkao wa mwili (posture) kila baada ya dakika 30

Hii kitaalamu inaitwa seat-stand posture yaani kukaa na kusimama. Maana ya hii ni kwamba kazi inakuwa inaendelea kama kawaida ila unaweza kufanya ukiwa umekaa au umesimama.

Unaweza kuketi wakati unachapa kwenye komputa yako na kuamua kusimama wakati unapangilia vitu vyako mezani. Tayari kuna meza na viti maalumu kwa ajili ya zoezi hili na zipo kampuni ambazo zimeshaanza kutumia vifaa hivi.

Ziko njia nyingine nyingi za kupunguza athari za kuketi muda mrefu kwa afya zetu.

Mwandishi wa makala hii ni Daktari bingwa wa fisiolojia ya homoni na mazoezi. Kupata ufahamu zaidi kuhusu mazoezi, mitindo ya maisha na afya tembelea youtube channel ya daktari hewani.
UNATAKA KUPATA HABARI NA BURUDANI FASTA BILA USUMBUFU ? BONYEZA HAPA

COMMENTS

Name

2014 Fifa World Cup 2baba 2face 50 Cent A.K.A A.Y Abbas Maziku Abdu Bonge Abdu Kiba Abela Music Abraham Poincheval ACT Adam Juma Adam Kuambiana Adam Mchomvu Adele adhabu Advert Afande Sele Africa African Blogger Awards African Celebs African News AFRIMA afrimama awards AFRIMMA Afya Afya Ya Mama Diamond Afya Ya Mapenzi Agatha Atiti Agnes Masogange Agness Masogange AIBU Aika AINEA Air Tanzania Airport Ajabu Ajali Ajira Aki Akon Akothee Al Shabaab Albino Album Cover Alice Kella Alikiba Aliko Dangote Ally Rehmtulah Amanda Poshy Amatus Liyumba Amazing Amber Lulu Amber rose Amina Sanani Amini AMVCA AWARDS 2014 Android Angelina Jolie Anniversary Apple Arianna Angel Arsenal Arusha Asha Baraka Aslay AT Audio August Alsina Augustine Mahiga Augustino Mrema Aunt Ezekiel Aunt Lulu Australia Avril Awards B.O.B B12 BAB J BABA DIAMOND BABA KANUMBA Babu Seya babu tale babu wa loliondo Baby Madaha BabyBoy Mapozy baeuty Banana Zoro banj Banky W Baraka Da Prince Baraka The Prince Barcelona Barnaba barua nzito Batuli BBA BBC Beef behind the scene Beka Ibrozama beki tatu Bella Belle 9 Ben Pol Benjamin Mkapa Benzema Best Nasso BET BET Awards BET Hip Hop Awards Betty Kyallo Beyonce Beyonce Knowle Biashara Bien Baraza Bifu BIG BROTHER Big Brother Hotshots Bikira Wa Kisukuma Bill Clinton Bill Nass Biography BirdMan Birthday Blac Jizzle Black Chyna Blue Ivy Bob Juniour Bob Marley Bobbi Kristina Brown Bobic Bondia Bonge la nyau Bongo Celebs Bongo Flava Bongo Fleva Bongo Movie Bongo Movies Bongo Swaggz Shindano Bongo Swaggz Tv Bongo Videos BongoSwaggz BongoSwaggz Play Store BOT Bow Wow Brad Pitt Brasil Breaking News Brown Mauzo Brown Punch (Bavoo) Brussels BS BSS BUNGE LA KATIBA. BUNGENI BURUDANI Bushoke Business C Pwaa C.E.O C9 Calisah Camon C9 CANCER Cannical Captain Komba Cars Carter V CashTime cazuza bon scott CCM Celebrities Celebrities Gossip Celebs CHADEMA Chagga Barbie Chagga Barbie na Zari The Boss Lady Changes Channel O Chege Cheka Chelsea Chibu Wayaya Chibu West Chicharito Chid Benz Chidi Mapenzi Chidinma Chin Bees China Chris Brown Chriss Brown christian bella Christian Ronaldo christina hewitt Chuchu Hans Ciara Clouds Fm Clouds Media Club La Liga Coke Studio Collabo Colonel Mustafa Comedy Coming Soon Corazon Kwamboka Coyo Mc Crimes Cristiano Ronaldo CSEE 2013 RESULTS Cyril Kamikaze d D banj d'banj D’banj damian soul Dance Dar es salaam darasa darasa la mapenzi darassa Dassy Amazing David Moyes Davido Davis mosha DAVIS MWAMUNYANGE Dawa Dawa Vidonda Vya Tumbo Dayna Death Decent Boy deddy Diamond Diamond na Zari Diamond Platnumz Diamond Platnumz Vs Davido Diana Kimaro DIDA Dillish Dipper Diva Diva Loveness Love divathebawse Dj Choka Dj D-Ommy Dj Fetty Dj Khaled Dj Sinyorita Dj Young Guru Dk. Vincet Mashinji Dkt. Asha-Rose Migiro Dog dogo janja Dogo Mfaume Don Jazzy Don Tach Donald Trump Doris Mollel Foundation Dr Cheni DR JOSE CHAMELEONE Dr. Dre Dr. John Pombe Magufuli Dr. Mwaka Dr. Slaa Drake Drinks DRM DSTv Dude DUDU BAYA dullayo Dully Sykes Dunga Duterte Dwayne Johnson EATV Awards Eddy Kenzo Education Edward Lowasa Elimu Elizabeth Michael Eminem Emmanuel Adebayor Emmanuel Mbasha Enos Olik Entertainment EPL Eric Omondi ESCROW Esma Platnumz Ethiopia Etihad Europe Evander Holyfield Events Exclusive Ezden Ezekiel Wenje Facebook Fadhili Awadh Fahyma Faiza FALLY IPUPA Fashion Fast & Furious Fast &Furious 7 Fast And Furious 8 Ferouz Fetty Feza Kessy Fid Q Fiesta 2013 FIESTA 2014 FIFA Filikunjombe First Godfrey Flaviana Matata Flora Mbasha Florah Mvungi Floyd Mayweather FM Academia Footballer Forads Forbes Fred Swagg Freeman Mbowe freemason freemason tanzania French Montana FUMANIZI Fuse ODG Future JNL G Nako G-Nako GABO ZIGAMBA Gadner Habash Galaxy Glass Gari Inauzwa gari mpya Geez Mabovu Gelly wa Rhymes GENEVIEVE Gentriez ghana Ghetto Kids Gift Gigy Money Girls global publisher Gmail Gnako Godbless Lema Godfather Godzilla Goodluck Gozbert Google Google Glass Gospel Gossip Grace Msale gwajima H BABA Habari Hakeem 5 Halima Kimwana Halima Mdee halimaty msodoki HAMISA MOBETO Hanscana Happiness Watimanywa Haristot Shungu Harmonize Harusi Hasheem Thabit Health Hemedi Hemedi Suleiman "PHD" Hillary Clinton Hip Hop HiPipo Awards HollyWood Homa La Jiji Hot In Town hot photo How To How to Love HTC Huddah HUSNA HUSNA MAULID Hussein Machozi Ian Ferrao Ice Prince Idris Sultan Imetosha Imetosha Campaign India Injili Instagram Interview iPhone iPhone 6 News iPhone 7 Irene Paul Irene Uwoya Iringa Isabela Issaya Mwita Charles Ivan Don Iyanya Izzo Business jack Cliff Jack Pemba Jackline Wolper jaguar Jah Prayzah Jakaya Mrisho Kikwete Jambo Squad Jamii January Makamba jaraja kubomoka jason deruLo jason deruro Jay C Jay Z JB Jini Jini Kabula Joh Makini Johari JOHN CENA John Legend john lennon John Mnyika John Woka Johnnie Walker Jokate jomo kenyata jordin sparcks Jose Mourinho Joseph Mbilinyi Joseph Msukuma Joti Joyheart Events JPEG Jude Okoye Juma Kaseja Juma Nature Jussie Smollett Justin Beiber Justin Bieber Jux K Lyamo K-LYN K.O K’naan kajala Kala Jeremiah Kalakala Kamikaze Kanga Moko Kanumba KANUMBA DAY Kanye West Karrueche Kassim Majaliwa Kayumba KCEE KCMC keisha Kelly Rowland Kenya kenya celebs Kesi Kevin-Prince Boateng Khadija Kopa Kiba Square Kidoa Kifo kigamboni Kigwangalla kikwete Kili Home Kilimanjaro Kilimanjaro Premium Lager Kim Kardashian Kimbunga Mchawi King Crazy GK King Kaka King Lawrence king majuto Kingunge Kitale Kizz Kiduku Klyn Koffi Olomide KOREA KR Mullah KTMA Kubenea kujinyonga kujiua Kupatwa Kwa Jua Kush Tracey Kutongoza Kylie Jenner LAANA LADY GAGA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lagos Laveda Le Mutuz leo Leo Mysterio Life Style Lij Michael LIL DRAINO lil kim Lil Wayne Linah Linex Lira Galore Live Updates Liverpool LOL Lola-Rae Lord Eyes Lost Airplane Love Love And Relationship Love Matters Love Story Love Tips Love Zone Lucci Luis Figo Luis Munana Lulu Lulu La Diva Lundenga Lupita Nyong'o Lynn M-Pawa M-Pesa m-rap MAAJABU Maalim Seif Sharif Hamad Mabeste MABOMU Mabruki Madam Rita Madawa ya Kulevya madee mademu Madhara Ya Mafikizolo MAFURIKO YA MAJI mafuriko ya mvua Magari Mazuri magazeti maimartha jesse Mainda Maisha Majanga Majay Makala makalio Makamba makavu live Make Love Makomando Malaika Malawi Malaysia malaysia airlines Malia Obama Malkiz MAMA DIAMOND MAMA KANUMBA Mama Lulu mama sharo milioneo Mama Wema Man Fongo Man u Man Utd Manchester City Manecky Mange Kimambi mangwea Manji Manny Pacquiao Mapenzi Maphorisa marilyn monroe Mario Balotelli Mark Zuckerberg Markson Beauty Products Marlaw Maromboso martin kadinda Masanja mkandamizaj Mashabiki masoud kipanya Mastaa Mastaa Bongo Master J matako bandia matokeo Matokeo Form Six Matokeo Kidato Cha Nne 2013 Matokeo Kidato Cha Nne 2015 Matonya MATUKIO Maua Maua Sama mauaji maximo MAYA Mayunga MB Dog mbagala Mbeya Mbinu Za Mapenzi MBWA WA WEMA Mc Dulla Mch. Christopher Mtikila Mechi Medicine Meek Mill Mekstar Melania Trump Menina Meninah Mesen Selekta Messenger Messi Mgomo Mh Job ndugai Mi-Casa Micah Boy Michael Jackson Michelle Obama Michepuko Michezo Mike Scotter Mike Tyson milipuko Millard Ayo Millen Magese Mimba Mirror Miss Bongo Movie Miss Bongo Muvi Miss Kilimanjaro 2016 Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 Miss KK Miss Rwanda Miss Tanzania Miss Tanzania 2014 Miss Uganda Miss World misukule Mkasa Mkasi mke wa sugu Mkubwa Na Wanawe Mkude Simba Mlela Mlimani City Mo Dewji mo music Mobile App Model Classic Models moe musa monalisa morogoro Mose Iyobo Moshi Movie Moyo Tara Flavour mpira Mr Blue Mr Flavour Mr Nice Mrema Mrembo Mrembo wa Wiki mrisho mpoto Msaga Sumu Msami Msiba Msigwa Mswaki MTANGAZAJI TIMES FM Mtoto Mtoto Wa Diamond mtoto wa nay wa mitego MTV MTV EMA MTV MAMA MUAJI Mubenga Muchoma Mugabe Muhammad Ali Multichoice Africa Muna Music MUSIC Mustapha Jaffer Sabodo Mwana FA Mwanafunzi Mwanamke MWANZA Mwasiti MZEE GURUMO Mzee Wa Upako Mzee Yussuf Mzee Yusuf Mziiki mzungu kichaa Nafca Nahreel Naj Nakaaya Nald Clever Nameless Nana Kwaku Bonsam NANDO Nape Nnauye Nash MC Nasibu Abdul Juma navy kenzo Nay Wamitego Nazizi Ndege Kupotea ndege ya malaysia Ndikumana Ndoa NEC NECTA Nedy Music Nelly Kamwelu Nelson Mandela Nemo New Blog New Maisha Club new movie New Product new ride New Track New Video News Ney Wa Mitego Neyo Ngasa ngono ya mdomo nguo za kubana Ngwea Nick Wa BongoSwaggz Nicki Minaj Nickson Lema niger celebs Nigeria Nikki Mbishi Nikki wa II Nikki Wa Pili Nisha Nisher Nisher Bye Nisher Entertainment Nissan Note Niva Nixl Carter Nokia Nonini Nora Nuh Mziwanda Nuhu Mziwanda nyerere Nyu Kid Obama Ochu Sheggy Octopizzo Odama Ojwang Olamide Ombeni Sefue Ommy Dimpoz Omotola Omotola Jalade Ekeinde One The Incredible Oprah Winfrey Ordinareh Bingwa Oscar Awards ostaz juma Ousmane Dembele P Diddy P Square P The Mc Pah One pakistan Pam D Pancho Chineke Panya Road Papa Francis Papa Wemba Papaa Masai Papi Kocha Paradise parliament Party Patcho Mwamba Patoranking Paul Kagame Paul Makonda Paul Okoye Paul Pogba Paul Walker Paula Penny Perfect Internet Peter Msechu Peter Okoye Petit Man Photo Photo Of The Day Picha picha za uchi picha chafu picha kli Picha Program Picha Ya Picha za mastaa Picha Za Matukio Picture pingu Pipi Pitbull PNC Political Issues Politics pombe Prezzo Princess Tiffah Privacy Priyanka Chopra Producer Prof. Ibrahaim Lipumba Profesa Jay Promo Promotion Q Chief Queen Darleen Queen Darling Quick Rocker R.I.P Raila Odinga rally Rama Dee Rammy Galis Range Rover Sport Raph Tz Ray Ray C Ray Vanny Raymond Rayuu RayVanny Read Madrid Real Madrid Recho Reekado Banks Regina Lowassa Reginald Mengi Rehab Relationship REMIX Rich Mavoko Rich People Richard BBA 2007 Richie Rick Ross Ridhiwani Kikwete Rihanna Rijo Voive RISPER Riyama Robin Thicke Rolene Strauss roma mkatoliki Romeo Romy Jons Rosa Ree Rose Muhando Rose Ndauka Rossie M Rostam Aziz Ruby RunTown Rwanda Sabby Sad News Saed Kubenea Safari Lager said fella Saint West Salam Tmk Salama Condom salama jabir Salamu Tmk Salha Israel Sallam Sk Salman Khan Salomon Kalou Sam Misago samaki wa ajabu Samantha Samatta SamBoy Samsung Samsung Galaxy S5 samweli sita Sarkodie Sasha Obama Sauda Mwilima Sauti Base Sauti Sol SBL sean kingston Secky Seki Selena Gomez Seline Selling Child Senga Serengeti Sergio Agguero Sergio Aguero Serikali Sexy Seyi Shay Shaa Shababi Shamsa Ford SHAMSA SORD Share SHARLEEN Sharo Millionea Sheddy Clever Shein Sherry Zuu Sheta Shetta Shevchenko Shilole Shocking News Sholo Mwamba Show Siasa SIKU KUU YA WAJINGA Simba Simulizi Sintah Siri Ya Mtungi Sitti Mtemvu Siwema Skendo snake bit Snoop Dogg Snura SOAP soccer Social Matters Social Networks SOKO LA KARUME Solution Somalia Somo Songa Sonko Sony South Africa spark Sport News Stamina Stan Bakora Stand United Stanna Stereo Steve Nyerere Steve RnB Steven Nyerere Stone Bone Stori Stori za Bongo Story Lounge suarez subaru Subaru Legacy Sudan SUGU Sumaye Super Nyota 2013 Swahili Jokes Swahili Music T-Pain T.I tahadhari Tajiri Talents Tamthilia tancredo neves tanesco Tangazo Tania tanz TANZANIA Tanzania Film Tanzania Music Tanzania News Tanzania One Tanzanian Tanzanian Actress Tanzanian music Tanzanian Rapper Tayo Folarin TB Joshua TBC Fm TBT TCRA TCU Teachers Technology Tecno Tekno Miles temba Tembo Tetesi TFF Thado The Game The Industry The Next Billionea Thea THT Tiara TID Tiffah Tigo Tiko Timbulo Times Fm Tinashe tip top connection Tiwa Savage tmk Togo Tottenham Hotspur Touch Phone TRA Trace TV trafiki trey songz Trick And Tips Tricks Tros Machine Trubadour George True Story Trust Trust Life TSH to USD Tuddy Thomas Tumaini University Tunda Tunda Man Tundu Lissu Tunisia Tupac Tusker Tuzo Tuzo za watu 2014 Twenty Percent Twerk Video Twitter Tyga U Heard ubakaji UCHAGUZI 2015 Uchawi Uchumi Supermarket ud Udaku Udaku Bongo Udaku Wa Bongo UDOM Uganda ugomvi ugomvi wa wema na kajala Uhuru Uhuru Kenyatta Uhusiano ukatili UKAWA Ukwa Umalaya UNESCO University News Unyama Urembo USA USA Celebs usagaji Usain Bolt Ushauri Usher Raymond Ushoga uswahilini uswazi Utabiri utajiri Utamu Vai Wa Ukweli Valentine Valentine's Day Van Persie Van Vicker vanessa chettle Vanessa Mdee Vannesa Mdee Venezuela VENGU VERA SIDIKA Vicent Kigosi vicent nyerere Vichekesho victoria kimani Video video queen Videos Vin Diesel visa vya mapenzi Vituko Vj Adams VJ Penny Vodacom vurugu Wahu WAJE Wale Walter Chilambo Wanawake Warning wasanii Wasira wastara Wayne Rooney wazungu WCB Wasafi Wedding Wedding Tanzania Weight Loss Welu Sengo WEMA Wema Sepetu wema sepetu alia wema sepetu kuzaa wema sepetu na ugumba Westgate Weusi Whatsapp Wildad William Bugeme Windhoek Beer Wise De Africa Wise One Witchcraft Witnesz wiz khalifa wizi Wizkid Wonder World News World Record Yamoto Band Yanga Yasinta Ycee Yemi Alade yesu bandia YMCMB Young D Young Dee: Situmii Madawa ya Kulevya ila Napiga Mtungi Kwa Sana Young Killer Young Money Yoweri Museveni yuzo mkali yvone chakachaka Z Anto z-anto zamaradi mketema Zanzibar Zari Zari All White Party Zari The Boss Lady Zimbabwe Zitto Aama Chama zitto kabwe Zitto Kabwe ACT Zlatan Ibrahimovic Zuhura Gora Zuleha Zuzu
false
ltr
item
BongoSwaggz.Com : Kuketi Muda Mrefu Kunaweza Kukusababishia Magonjwa Haya.
Kuketi Muda Mrefu Kunaweza Kukusababishia Magonjwa Haya.
https://4.bp.blogspot.com/-Lk75A4GsUbo/V5rri_xWk5I/AAAAAAAALXQ/xkQZC5St7bk_qiBR7i2Tijo8SGXQ65uUQCLcB/s1600/salud_laboral_mala_postura.png
https://4.bp.blogspot.com/-Lk75A4GsUbo/V5rri_xWk5I/AAAAAAAALXQ/xkQZC5St7bk_qiBR7i2Tijo8SGXQ65uUQCLcB/s72-c/salud_laboral_mala_postura.png
BongoSwaggz.Com
http://www.bongoswaggz.com/2016/07/kuketi-muda-mrefu-kunaweza.html
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/2016/07/kuketi-muda-mrefu-kunaweza.html
true
371784233821042440
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy