Chadema Sasa Yaja na Operesheni Ukuta

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezindua operesheni mpya iliyopewa jina la Umoja wa...

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezindua operesheni mpya iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Operesheni hiyo inakwenda sambamba na uzinduzi wa mikutano ya hadhara nchi nzima, ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Hayo yametokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa siku nne mfululizo jijini Dar es Salaam na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekezwa na chama.

Pamoja na mambo mengine, chama hicho kimesema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini, kiliyodai kuwa yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli.

Akitangaza uamuzi huo Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alisema Kamati Kuu imejadili kwa kina hali ya kisiasa nchini na kutoa maazimio hayo.

“Tangu kuanza kwa utawala wa awamu ya tano, kuna matukio mbalimbali ya kubinya demokrasia na kuua dhana ya utawala bora, na yapo makundi ambayo tayari yameshaumizwa, huku Watanzania wengi wakikaa kimya kwa sababu wao si sehemu ya kundi lililominywa.

“Kwa kuwa wewe tayari umeshafikiwa, hauna budi kujenga Ukuta ili kuzuia wengine wasidhurike na utawala huu. Kwa kuwa wewe hujafikiwa na ndiyo maana husemi wenzako wanapofikiwa, basi njoo tujenge Ukuta ili ukifikiwa awepo wa kusema,” alisema Mbowe.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema suala la kujenga Ukuta halitachagua itikadi za chama wala dini.

Kutokana na hilo, aliwataka viongozi wa dini zote pamoja na Watanzania wapenda amani, kuungana na chama hicho kujenga Ukuta ili kuzuia uchumi kuporomoka.

“Njoo tujenge Ukuta kuzuia udikteta huu, tujenge Ukuta tuilinde Katiba yetu… Ukuta huu ni wa wananchi wote bila kujali dini, kabila, chama cha siasa au rangi,” alisema Mbowe.

Akizungumzia chimbuko la Ukuta, Mbowe alisema umetokana na Rais Magufuli kupiga marufuku safari zote za nje kwa watumishi wa umma, kuamuru Mahakama Kuu iwahukumu wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi ili Serikali ishinde.

Alisema nyingine ni Serikali kuingilia Bunge na kupanga wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, kuzuia matangazo ya moja kwa moja (live) ya Bunge kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) na vituo binafsi pamoja na wabunge wa upinzani kunyanyaswa na hata hotuba zao kufutwa kinyume na kanuni za Bunge.

Aidha Mbowe alisema sababu zilizowasukuma kuanzisha Ukuta ni pamoja na mabalozi na wanadiplomasia kuzuiliwa kukutana na viongozi wa kisiasa bila kibali cha Serikali, watumishi wa umma kufukuzwa ovyo bila utaratibu kwa kisingizio cha kutumbua majipu bila kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma na mawakili kuunganishwa kwenye kesi za wateja wao wanapokwenda kuwatetea.

Mbowe alitaja sababu nyingine kuwa ni Serikali kuendeshwa kwa matamko badala ya Katiba na sheria, Serikali kuwafukuza na kuwadhalilisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku.

Walimu kukatwa mishahara iwapo dawati litavunjika kwenye shule yake, kupotezwa kwa wana-CCM ambao watapinga kauli ya mwenyekiti au kuwa na maoni tofauti, unyanyasaji na udhalilishaji wa viongozi wa dini na wananchi wa Zanzibar ni miongoni mwa sababu alizotaja Mbowe.

“Historia inaonyesha duniani kote hakuna ambako utawala uliwahi kuushinda ukuta wa wananchi, na hii ndiyo nguvu ya umma, kila mmoja achukue hatua popote alipo kujenga Ukuta,” alisema.

Kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara Septemba Mosi, Mbowe alisema Kamati Kuu imeagiza ngazi zote za chama kuanzia ya msingi, kata, majimbo, wilaya, mikoa, kanda, mabaraza na taifa kukaa na kufanya maandalizi ya mikutano hiyo nchi nzima.

Katika azimio jingine, Mbowe alisema Kamati Kuu imewataka wanasheria wote wa chama kuchukua hatua zote za kisheria kwa mambo yote yaliyotokea juu ya uvunjaji wa Katiba.

“Kamati Kuu imeagiza wanasheria wote wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu, kuangalia haki kupitia mahakama na kuhoji tafsiri ya vifungu vya sheria vilivyovunjwa,” alisema Mbowe.

Kutokana na maazimio hayo, Mbowe alisema inawezekana wasiwe salama, lakini wameamua kumweleza Rais Magufuli mambo anayoyafanya kwa sababu washauri wake wameshindwa.

“Wote kama taifa tuna wajibu wa kuchukua hatua, na pale tunaponyamazishwa na kukubali tutakuwa tunaharibu nchi.

“Inawezekana pengine washauri wake hawamwelezi, sisi tunamweleza na inawezekana tusiwe salama na hatimaye nchi hii haitakuwa salama.

“Tangu Uchaguzi Mkuu ulipokwisha hatujawahi kufanya mkutano hata mmoja, lakini rais yeye anaona kwake ni halali. Sisi tukikaa hivi hatutajenga taifa la demokrasia.

“Rais hajanyimwa kufanya kazi zake, yeye si malaika, tutamkosoa tu pale atakapokosea na kumpongeza pale anapofanya vizuri,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa itakuwaje mikutano hiyo ikipambana na nguvu ya dola, alisema tangu Chadema ilipoanzishwa mwaka 1992, ilipitia hatua mbalimbali zenye maumivu mengi na haikuwa fadhila ya mtu.

“Wako waliopoteza maisha wakipigania chama hiki, wengine wamekuwa walemavu, wengine wamepata madhila mengi, hivyo ujenzi huu wa demokrasia si kwa faida yetu lakini kwa faida yenu, watoto wenu na watoto wa watoto wenu.

“Tunatambua uwepo wa dola, sasa tukisema tuiogope dola halafu taifa liporomoke? Maswali mliyouliza waandishi wa habari yamejaa hofu… tumejenga taifa lenye woga na hofu, yaani kwa kuwa mtu mmoja kasema basi tutulie tu?” alihoji Mbowe.

Alisema waliamua kukaa kimya tangu Novemba mwaka jana, huku wakiwazuia vijana kutofanya maandamano, lakini bado watawala hawakuliona hilo.

“Sisi tumesaidia kuwepo amani ya nchi hii, maana tangu uchaguzi wa mwaka jana tumekuwa tukiwazuia vijana wetu kutofanya maandamano, tukakaa kimya kwa lengo la kuipa muda Serikali hii, lakini tunaona ubabe tu.

“Hatujawa waoga na hatutakuwa waoga, ila tunafanya kila jambo kwa tahadhari, tukiendelea kukaa kimya tutakuwa hatujautendea haki wajibu wetu kama viongozi,” alisema.

-Mtanzania UNATAKA KUPATA HABARI NA BURUDANI FASTA BILA USUMBUFU ? BONYEZA HAPA

COMMENTS

Name

2014 Fifa World Cup 2baba 2face 50 Cent A.K.A A.Y Abbas Maziku Abdu Bonge Abdu Kiba Abela Music Abraham Poincheval ACT Adam Juma Adam Kuambiana Adam Mchomvu Adele adhabu Advert Afande Sele Africa African Blogger Awards African Celebs African News AFRIMA afrimama awards AFRIMMA Afya Afya Ya Mama Diamond Afya Ya Mapenzi Agatha Atiti Agnes Masogange Agness Masogange AIBU Aika AINEA Air Tanzania Airport Ajabu Ajali Ajira Aki Akon Akothee Al Shabaab Albino Album Cover Alice Kella Alikiba Aliko Dangote Ally Rehmtulah Amanda Poshy Amatus Liyumba Amazing Amber Lulu Amber rose Amina Sanani Amini AMVCA AWARDS 2014 Android Angelina Jolie Anniversary Apple Arianna Angel Arsenal Arusha Asha Baraka Aslay AT Audio August Alsina Augustine Mahiga Augustino Mrema Aunt Ezekiel Aunt Lulu Australia Avril Awards B.O.B B12 BAB J BABA DIAMOND BABA KANUMBA Babu Seya babu tale babu wa loliondo Baby Madaha BabyBoy Mapozy baeuty Banana Zoro banj Banky W Baraka Da Prince Baraka The Prince Barcelona Barnaba barua nzito Batuli BBA BBC Beef behind the scene Beka Ibrozama beki tatu Bella Belle 9 Ben Pol Benjamin Mkapa Benzema Best Nasso BET BET Awards BET Hip Hop Awards Betty Kyallo Beyonce Beyonce Knowle Biashara Bien Baraza Bifu BIG BROTHER Big Brother Hotshots Bikira Wa Kisukuma Bill Clinton Bill Nass Biography BirdMan Birthday Blac Jizzle Black Chyna Blue Ivy Bob Juniour Bob Marley Bobbi Kristina Brown Bobic Bondia Bonge la nyau Bongo Celebs Bongo Flava Bongo Fleva Bongo Movie Bongo Movies Bongo Swaggz Shindano Bongo Swaggz Tv Bongo Videos BongoSwaggz BongoSwaggz Play Store BOT Bow Wow Brad Pitt Brasil Breaking News Brown Mauzo Brown Punch (Bavoo) Brussels BS BSS BUNGE LA KATIBA. BUNGENI BURUDANI Bushoke Business C Pwaa C.E.O C9 Calisah Camon C9 CANCER Cannical Captain Komba Cars Carter V CashTime cazuza bon scott CCM Celebrities Celebrities Gossip Celebs CHADEMA Chagga Barbie Chagga Barbie na Zari The Boss Lady Changes Channel O Chege Cheka Chelsea Chibu Wayaya Chibu West Chicharito Chid Benz Chidi Mapenzi Chidinma Chin Bees China Chris Brown Chriss Brown christian bella Christian Ronaldo christina hewitt Chuchu Hans Ciara Clouds Fm Clouds Media Club La Liga Coke Studio Collabo Colonel Mustafa Comedy Coming Soon Corazon Kwamboka Coyo Mc Crimes Cristiano Ronaldo CSEE 2013 RESULTS Cyril Kamikaze d D banj d'banj D’banj damian soul Dance Dar es salaam darasa darasa la mapenzi darassa Dassy Amazing David Moyes Davido Davis mosha DAVIS MWAMUNYANGE Dawa Dawa Vidonda Vya Tumbo Dayna Death Decent Boy deddy Diamond Diamond na Zari Diamond Platnumz Diamond Platnumz Vs Davido Diana Kimaro DIDA Dillish Dipper Diva Diva Loveness Love divathebawse Dj Choka Dj D-Ommy Dj Fetty Dj Khaled Dj Sinyorita Dj Young Guru Dk. Vincet Mashinji Dkt. Asha-Rose Migiro Dog dogo janja Dogo Mfaume Don Jazzy Don Tach Donald Trump Doris Mollel Foundation Dr Cheni DR JOSE CHAMELEONE Dr. Dre Dr. John Pombe Magufuli Dr. Mwaka Dr. Slaa Drake Drinks DRM DSTv Dude DUDU BAYA dullayo Dully Sykes Dunga Duterte Dwayne Johnson EATV Awards Eddy Kenzo Education Edward Lowasa Elimu Elizabeth Michael Eminem Emmanuel Adebayor Emmanuel Mbasha Enos Olik Entertainment EPL Eric Omondi ESCROW Esma Platnumz Ethiopia Etihad Europe Evander Holyfield Events Exclusive Ezden Ezekiel Wenje Facebook Fadhili Awadh Fahyma Faiza FALLY IPUPA Fashion Fast & Furious Fast &Furious 7 Fast And Furious 8 Ferouz Fetty Feza Kessy Fid Q Fiesta 2013 FIESTA 2014 FIFA Filikunjombe First Godfrey Flaviana Matata Flora Mbasha Florah Mvungi Floyd Mayweather FM Academia Footballer Forads Forbes Fred Swagg Freeman Mbowe freemason freemason tanzania French Montana FUMANIZI Fuse ODG Future JNL G Nako G-Nako GABO ZIGAMBA Gadner Habash Galaxy Glass Gari Inauzwa gari mpya Geez Mabovu Gelly wa Rhymes GENEVIEVE Gentriez ghana Ghetto Kids Gift Gigy Money Girls global publisher Gmail Gnako Godbless Lema Godfather Godzilla Goodluck Gozbert Google Google Glass Gospel Gossip Grace Msale gwajima H BABA Habari Hakeem 5 Halima Kimwana Halima Mdee halimaty msodoki HAMISA MOBETO Hanscana Happiness Watimanywa Haristot Shungu Harmonize Harusi Hasheem Thabit Health Hemedi Hemedi Suleiman "PHD" Hillary Clinton Hip Hop HiPipo Awards HollyWood Homa La Jiji Hot In Town hot photo How To How to Love HTC Huddah HUSNA HUSNA MAULID Hussein Machozi Ian Ferrao Ice Prince Idris Sultan Imetosha Imetosha Campaign India Injili Instagram Interview iPhone iPhone 6 News iPhone 7 Irene Paul Irene Uwoya Iringa Isabela Issaya Mwita Charles Ivan Don Iyanya Izzo Business jack Cliff Jack Pemba Jackline Wolper jaguar Jah Prayzah Jakaya Mrisho Kikwete Jambo Squad Jamii January Makamba jaraja kubomoka jason deruLo jason deruro Jay C Jay Z JB Jini Jini Kabula Joh Makini Johari JOHN CENA John Legend john lennon John Mnyika John Woka Johnnie Walker Jokate jomo kenyata jordin sparcks Jose Mourinho Joseph Mbilinyi Joseph Msukuma Joti Joyheart Events JPEG Jude Okoye Juma Kaseja Juma Nature Jussie Smollett Justin Beiber Justin Bieber Jux K Lyamo K-LYN K.O K’naan kajala Kala Jeremiah Kalakala Kamikaze Kanga Moko Kanumba KANUMBA DAY Kanye West Karrueche Kassim Majaliwa Kayumba KCEE KCMC keisha Kelly Rowland Kenya kenya celebs Kesi Kevin-Prince Boateng Khadija Kopa Kiba Square Kidoa Kifo kigamboni Kigwangalla kikwete Kili Home Kilimanjaro Kilimanjaro Premium Lager Kim Kardashian Kimbunga Mchawi King Crazy GK King Kaka King Lawrence king majuto Kingunge Kitale Kizz Kiduku Klyn Koffi Olomide KOREA KR Mullah KTMA Kubenea kujinyonga kujiua Kupatwa Kwa Jua Kush Tracey Kutongoza Kylie Jenner LAANA LADY GAGA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lagos Laveda Le Mutuz leo Leo Mysterio Life Style Lij Michael LIL DRAINO lil kim Lil Wayne Linah Linex Lira Galore Live Updates Liverpool LOL Lola-Rae Lord Eyes Lost Airplane Love Love And Relationship Love Matters Love Story Love Tips Love Zone Lucci Luis Figo Luis Munana Lulu Lulu La Diva Lundenga Lupita Nyong'o Lynn M-Pawa M-Pesa m-rap MAAJABU Maalim Seif Sharif Hamad Mabeste MABOMU Mabruki Madam Rita Madawa ya Kulevya madee mademu Madhara Ya Mafikizolo MAFURIKO YA MAJI mafuriko ya mvua Magari Mazuri magazeti maimartha jesse Mainda Maisha Majanga Majay Makala makalio Makamba makavu live Make Love Makomando Malaika Malawi Malaysia malaysia airlines Malia Obama Malkiz MAMA DIAMOND MAMA KANUMBA Mama Lulu mama sharo milioneo Mama Wema Man Fongo Man u Man Utd Manchester City Manecky Mange Kimambi mangwea Manji Manny Pacquiao Mapenzi Maphorisa marilyn monroe Mario Balotelli Mark Zuckerberg Markson Beauty Products Marlaw Maromboso martin kadinda Masanja mkandamizaj Mashabiki masoud kipanya Mastaa Mastaa Bongo Master J matako bandia matokeo Matokeo Form Six Matokeo Kidato Cha Nne 2013 Matokeo Kidato Cha Nne 2015 Matonya MATUKIO Maua Maua Sama mauaji maximo MAYA Mayunga MB Dog mbagala Mbeya Mbinu Za Mapenzi MBWA WA WEMA Mc Dulla Mch. Christopher Mtikila Mechi Medicine Meek Mill Mekstar Melania Trump Menina Meninah Mesen Selekta Messenger Messi Mgomo Mh Job ndugai Mi-Casa Micah Boy Michael Jackson Michelle Obama Michepuko Michezo Mike Scotter Mike Tyson milipuko Millard Ayo Millen Magese Mimba Mirror Miss Bongo Movie Miss Bongo Muvi Miss Kilimanjaro 2016 Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 Miss KK Miss Rwanda Miss Tanzania Miss Tanzania 2014 Miss Uganda Miss World misukule Mkasa Mkasi mke wa sugu Mkubwa Na Wanawe Mkude Simba Mlela Mlimani City Mo Dewji mo music Mobile App Model Classic Models moe musa monalisa morogoro Mose Iyobo Moshi Movie Moyo Tara Flavour mpira Mr Blue Mr Flavour Mr Nice Mrema Mrembo Mrembo wa Wiki mrisho mpoto Msaga Sumu Msami Msiba Msigwa Mswaki MTANGAZAJI TIMES FM Mtoto Mtoto Wa Diamond mtoto wa nay wa mitego MTV MTV EMA MTV MAMA MUAJI Mubenga Muchoma Mugabe Muhammad Ali Multichoice Africa Muna Music MUSIC Mustapha Jaffer Sabodo Mwana FA Mwanafunzi Mwanamke MWANZA Mwasiti MZEE GURUMO Mzee Wa Upako Mzee Yussuf Mzee Yusuf Mziiki mzungu kichaa Nafca Nahreel Naj Nakaaya Nald Clever Nameless Nana Kwaku Bonsam NANDO Nape Nnauye Nash MC Nasibu Abdul Juma navy kenzo Nay Wamitego Nazizi Ndege Kupotea ndege ya malaysia Ndikumana Ndoa NEC NECTA Nedy Music Nelly Kamwelu Nelson Mandela Nemo New Blog New Maisha Club new movie New Product new ride New Track New Video News Ney Wa Mitego Neyo Ngasa ngono ya mdomo nguo za kubana Ngwea Nick Wa BongoSwaggz Nicki Minaj Nickson Lema niger celebs Nigeria Nikki Mbishi Nikki wa II Nikki Wa Pili Nisha Nisher Nisher Bye Nisher Entertainment Nissan Note Niva Nixl Carter Nokia Nonini Nora Nuh Mziwanda Nuhu Mziwanda nyerere Nyu Kid Obama Ochu Sheggy Octopizzo Odama Ojwang Olamide Ombeni Sefue Ommy Dimpoz Omotola Omotola Jalade Ekeinde One The Incredible Oprah Winfrey Ordinareh Bingwa Oscar Awards ostaz juma Ousmane Dembele P Diddy P Square P The Mc Pah One pakistan Pam D Pancho Chineke Panya Road Papa Francis Papa Wemba Papaa Masai Papi Kocha Paradise parliament Party Patcho Mwamba Patoranking Paul Kagame Paul Makonda Paul Okoye Paul Pogba Paul Walker Paula Penny Perfect Internet Peter Msechu Peter Okoye Petit Man Photo Photo Of The Day Picha picha za uchi picha chafu picha kli Picha Program Picha Ya Picha za mastaa Picha Za Matukio Picture pingu Pipi Pitbull PNC Political Issues Politics pombe Prezzo Princess Tiffah Privacy Priyanka Chopra Producer Prof. Ibrahaim Lipumba Profesa Jay Promo Promotion Q Boy Q Chief Queen Darleen Queen Darling Quick Rocker R.I.P Raila Odinga rally Rama Dee Rammy Galis Range Rover Sport Raph Tz Ray Ray C Ray Vanny Raymond Rayuu RayVanny Read Madrid Real Madrid Recho Reekado Banks Regina Lowassa Reginald Mengi Rehab Relationship REMIX Rich Mavoko Rich People Richard BBA 2007 Richie Rick Ross Ridhiwani Kikwete Rihanna Rijo Voive RISPER Riyama Robin Thicke Rolene Strauss roma mkatoliki Romeo Romy Jons Rosa Ree Rose Muhando Rose Ndauka Rossie M Rostam Aziz Ruby RunTown Rwanda Sabby Sad News Saed Kubenea Safari Lager said fella Saint West Salam Tmk Salama Condom salama jabir Salamu Tmk Salha Israel Sallam Sk Salman Khan Salomon Kalou Sam Misago samaki wa ajabu Samantha Samatta SamBoy Samsung Samsung Galaxy S5 samweli sita Sarkodie Sasha Obama Sauda Mwilima Sauti Base Sauti Sol SBL sean kingston Secky Seki Selena Gomez Seline Selling Child Senga Serengeti Sergio Agguero Sergio Aguero Serikali Sexy Seyi Shay Shaa Shababi Shamsa Ford SHAMSA SORD Share SHARLEEN Sharo Millionea Sheddy Clever Shein Sherry Zuu Sheta Shetta Shevchenko Shilole Shocking News Sholo Mwamba Show Siasa SIKU KUU YA WAJINGA Simba Simulizi Sintah Siri Ya Mtungi Sitti Mtemvu Siwema Skendo snake bit Snoop Dogg Snura SOAP soccer Social Matters Social Networks SOKO LA KARUME Solution Somalia Somo Songa Sonko Sony South Africa spark Sport News Stamina Stan Bakora Stand United Stanna Stereo Steve Nyerere Steve RnB Steven Nyerere Stone Bone Stori Stori za Bongo Story Lounge suarez subaru Subaru Legacy Sudan SUGU Sumaye Super Nyota 2013 Swahili Jokes Swahili Music T-Pain T.I tahadhari Tajiri Talents Tamthilia tancredo neves tanesco Tangazo Tania tanz TANZANIA Tanzania Film Tanzania Music Tanzania News Tanzania One Tanzanian Tanzanian Actress Tanzanian music Tanzanian Rapper Tayo Folarin TB Joshua TBC Fm TBT TCRA TCU Teachers Technology Tecno Tekno Miles temba Tembo Tetesi TFF Thado The Game The Industry The Next Billionea Thea THT Tiara TID Tiffah Tigo Tiko Timbulo Times Fm Tinashe tip top connection Tiwa Savage tmk Togo Tottenham Hotspur Touch Phone TRA Trace TV trafiki trey songz Trick And Tips Tricks Tros Machine Trubadour George True Story Trust Trust Life TSH to USD Tuddy Thomas Tumaini University Tunda Tunda Man Tundu Lissu Tunisia Tupac Tusker Tuzo Tuzo za watu 2014 Twenty Percent Twerk Video Twitter Tyga U Heard ubakaji UCHAGUZI 2015 Uchawi Uchumi Supermarket ud Udaku Udaku Bongo Udaku Wa Bongo UDOM Uganda ugomvi ugomvi wa wema na kajala Uhuru Uhuru Kenyatta Uhusiano ukatili UKAWA Ukwa Umalaya UNESCO University News Unyama Urembo USA USA Celebs usagaji Usain Bolt Ushauri Usher Raymond Ushoga uswahilini uswazi Utabiri utajiri Utamu Vai Wa Ukweli Valentine Valentine's Day Van Persie Van Vicker vanessa chettle Vanessa Mdee Vannesa Mdee Venezuela VENGU VERA SIDIKA Vicent Kigosi vicent nyerere Vichekesho victoria kimani Video video queen Videos Vin Diesel visa vya mapenzi Vituko Vj Adams VJ Penny Vodacom vurugu Wahu WAJE Wale Walter Chilambo Wanawake Warning wasanii Wasira wastara Wayne Rooney wazungu WCB Wasafi Wedding Wedding Tanzania Weight Loss Welu Sengo WEMA Wema Sepetu wema sepetu alia wema sepetu kuzaa wema sepetu na ugumba Westgate Weusi Whatsapp Wildad William Bugeme Windhoek Beer Wise De Africa Wise One Witchcraft Witnesz wiz khalifa wizi Wizkid Wonder World News World Record Yamoto Band Yanga Yasinta Ycee Yemi Alade yesu bandia YMCMB Young D Young Dee: Situmii Madawa ya Kulevya ila Napiga Mtungi Kwa Sana Young Killer Young Money Yoweri Museveni yuzo mkali yvone chakachaka Z Anto z-anto zamaradi mketema Zanzibar Zari Zari All White Party Zari The Boss Lady Zimbabwe Zitto Aama Chama zitto kabwe Zitto Kabwe ACT Zlatan Ibrahimovic Zuhura Gora Zuleha Zuzu
false
ltr
item
BongoSwaggz.Com : Chadema Sasa Yaja na Operesheni Ukuta
Chadema Sasa Yaja na Operesheni Ukuta
https://3.bp.blogspot.com/-B09_pzMOrqc/V5m74JI2l1I/AAAAAAAALV0/4yTMYAdISSIXISt9DDJsuSU6KIUlWzI4wCLcB/s640/chadema.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-B09_pzMOrqc/V5m74JI2l1I/AAAAAAAALV0/4yTMYAdISSIXISt9DDJsuSU6KIUlWzI4wCLcB/s72-c/chadema.jpg
BongoSwaggz.Com
http://www.bongoswaggz.com/2016/07/chadema-sasa-yaja-na-operesheni-ukuta.html
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/2016/07/chadema-sasa-yaja-na-operesheni-ukuta.html
true
371784233821042440
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy