Advert

Breaking News

Mohammed Morsi Ahukumiwa Kifungo cha Maisha

Mahakama ya Misri imempatia kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Kiislamu Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi.

Ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshtumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar.

Wakili wa Bw Morsi amesema kuwa aliwachiliwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu.

Wengine ni waandishi wawili wa Aljazeera ambao walihukumiwa kifo wakiwa hawako mahakamani.

Hata hivyo kiongozi huyo wa zamani ana uwezo wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama unaojiri wakati ambapo sekta ya mahakama ya Misri inaendelea kukosolewa na makundi ya wanaharakati duniani.

-BBC
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.