Advert

Breaking News

Yamoto Band Na Kayumba Wameandika Wimbo Ujao Wa Shaa Uitwao ‘Sawa’

Kundi la Yamoto Band pamoja na mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2015, Kayumba, wameshirikiana kuandika wimbo ujao wa Shaa uitwao ‘Sawa.’


10296857_428252300717140_694490122_n
Shaa aliambia Bongo5 kuwa akiwa chini ya usimamizi wa Said Fella, amekuwa akikutana na vijana hao mara kwa mara kwenye studio za Mkubwa na Wanawe.
“Niko chini ya usimamizi wa Mkubwa na Wanawe kwahiyo nikifika pale wananiambia ‘dada Shaa tumekuandikia hii, hebu sikia.’ Nawasikilizaga kwasababu soko sasa hivi lipo kiujana zaidi, kwahiyo nikiona kwamba vijana wanajua soko liko wapi nawasikiliza,” aliongeza.
Video ya wimbo huo tayari imefanyika na kuongozwa na Justin Campus. Video na wimbo huo vitatoka hivi karibuni.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.