Namuombea Jack Patrick Atoke Jela Mapema - Vanessa Mdee - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Namuombea Jack Patrick Atoke Jela Mapema - Vanessa Mdee

Mwanamuziki Vanessa Mdee amesema anamuombea Jack Patrick atoke jela mapema.
Jack aliyefungwa jela nchini China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aliwahi kuwa mpenzi wa Jux, ambaye kwa sasa ni boyfriend wa muimbaji huyo wa Niroge.

“Namuombea atoke jela mapema, nadhani matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo tunafikiria sisi,” ameiambia Global TV.

“Sidhani hata kama huwa ananifikiria, nadhani anafikiria familia yake na hali ambayo anakosa maisha ya kawaida,” aliongeza.

Vanessa aliyeachia wimbo mpya Niroge hivi karibuni alisisitiza kuwa hakumuibia Jack bwana (Jux) na kwamba alikuwa akimfahamu msichana huyo kama model wengine.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.