Advert

Breaking News

Mwasiti Ajitetea Kufulia Kimuziki.

STAA Mkongwe wa Bongo Fleva kutoka Jumba la Kuibua Vipaji vya Kuimba (THT), Mwasiti Almasi amefungukia maisha yake kimuziki kwamba hajafulia kwani kazi zake bado zinaendelea kuchezwa hasa mikoani.

Akichonga na Showbiz Xtra Mwasiti anayebamba na Ngoma ya Sema Naye alisema, mashabiki wameshazoea kumuona akiimba muziki wa aina moja na katika wimbo wake mpya huo amebadilika na ndiyo chanzo cha wengi kutompokea vema.

“Bado nafanya muziki na kwa sasa nina Wimbo wa Sema Naye japokuwa kwa hapa Dar ni kweli haujapokelewa vizuri lakini mikoani unachezwa sana tu,” alisema Mwasiti.
Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.