Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Usharobaro wamtokea puani Stan Bakora


Usharobaro umemtokea puani komediani wa Bongo, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’ baada ya kudondoka na kuumia mguu wa kulia wakati akifanya mazoezi ya kutumia Cyboard (Saibodi).

Ishu nzima ilitokea wiki iliyopita katika moja ya duka la nguo lililopo Kinondoni, Dar baada ya kupiga mwereka wa kufa mtu na kujikuta akianguka kama mkungu wa ndizi kutoka juu ya mgomba kisha kuumia mguu.
Akiwa kwenye Cyboard.
“Hicho kidude, kwangu ni kigeni ndiyo nilikuwa nakijaribisha nione inakuwaje ndipo nilipoanguka kama mara mbili hivi na kuumia mguu wa kulia, kiukweli kimenitoa ushamba,” alisema Stan Bakola. Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.