Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Mtandao wa Facebook Umezindua Vitufe (Emoji) 5 Mpya, Zione Hapa


Kuanzia leo mtandao wa kijamii wa Facebook umezindua vitufe (emojis) 5 vipya ilikufanikisha watumiaji wa mtandao huu kujieleza kwa kutoa maoni yao kwa usahihi zaidi ima wamefurahia jambo ama hata wamelikataa kwa kubofya picha inayoambatanisha na maoni yao. Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Facebook bwana Mark Zuckerberg amesema kuwa watumiaji bilioni 1.5 wa mtandao huo wataanza a kutumia vitufe hivyo vipya leo(jumatano).

Vitufe hivyo vipya vina picha ya "wow(Furahia)", "penda", "haha(Cheka)", " huzuni" na"yakasirisha". Kitufe cha ''Like'' ambacho ndicho kilikuwa kibwagizo cha Facebook katika kipindi cha miaka 7 kimesalia hapo kama nembo ya kuwasaidia watumizi kujieleza zaidi katika mtandao wa Facebook alisema bwana Zuckerberg kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wake wa Facebook.

Unaweza Kujaribu Emoji Hizi Bofya Hapa

''Bila shaka ninafahamu kuwa sio habari zote unazozipata kupitia kwenye mtandao wa Facebook ni za kufurahisha (like) ndio sababu tumekupa hizi zingine kukuwezesha kujieleza kwa njia sahihi zaidi katika Faceboook. ''Kwa mtazamo wangu kitufe cha kupenda ndicho kilichotumika sana haswa katika kipindi cha majaribio'' alisema mkurugenzi huyo wa facebook. Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.