Advert

Download Nyimbo Mpya

Breaking News

Arsenal Wanunua Kiungo wa FC Basel

Elneny
Elneny anaweza kuchezea Arsenal dhidi ya Stoke Jumapili
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.

Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.

Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: "Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.”
Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea msimu wa 2013-14. Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram << na >> PlayStore << Kupata Habari na Burudani Fasta Kila Time.

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.