Advert

Breaking News

Nisha Na Mpenzi Wake Baraka Da prince Pachimbika

STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na mpenzi wake, Baraka Da Prince wameingia kwenye gogoro zito baada ya mwanaume huyo kuripotiwa kutoka kimapenzi na muigizaji mwingine, Husna Idd ‘Sajent’.
Katika mawasiliano kati ya gazeti hili na Nisha juzikati, muigizaji huyo aliiweka simu yake hewani na mwandishi wetu kusikia wawili hao wakigombana huku Baraka akitukana matusi ya nguoni akiwalenga waandishi walioibua stori hiyo, akijitetea kwamba haikuwa kweli.
“Nimemuuliza Baraka kuhusu hiyo ishu, amekuja juu sana yaani pamechimbika, sipendi kupaniki wala sitaki kugombana na Sajent kisa mwanaume, kwa sababu sisi sote ni wanawake, kikubwa ninachoangalia ni jinsi gani mwanaume huyu anavyoniheshimu na najua ninachopata kwake, kweli tumetibuana kutokana na hilo ila najua Mungu ndiye anayejua ukweli wote,” alisema Nisha.

-GPL
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.