MO DEWJI APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dew...

IMG_3351
Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog team
MFANYABIASHARA na  mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya  "Forbes Africa Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mfanyabiashara huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya 1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai  na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari anashea ya asilimia 40 ya soko.
Mo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.
Aidha wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.
Akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
Mo ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini.
IMG_3317
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Alisema ajira 26,000 zimegusa watu wengi nchini na kwamba  ana matumaini makubwa ya siku za usoni kutoa ajira zaidi kutokana na biashara zake kuendelea kukua.
"Heshima yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada wala kugusa watu masikini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuta ya kupikia na maji ya kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila nyakati katika siku.
"Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa bei yenye unafuu mkubwa, mathalani tunauza maji kwa bei chini ya dola moja kwa shilingi za Kitanzania 200, hakuna hata Ulaya, nina kiwanda cha khanga na vitenge ambacho malighafi zake zote ni za Kitanzania, hivyo kuna kusaidia serikali kwa kulipa kodi ipasavyo, lakini pia kusaidia moja kwa moja ajira za Watanzania walio wengi ambao tatizo lao kubwa katika kundi la vijana ni ajira"
Alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza baba yake kwa kumwita mjasiriamali shujaa ambaye alitoka kuanzia dereva wa malori baada ya kuhitimu kidato cha nne mwishoni mwa miaka ya 1960 hadi kufikia ubilionea. Alisema alipata maono ya utajiri hasa kutoka kwa baba yake huyo aliyekuwa akimshirikisha biashara tangu akiwa mdogo.
“Mwanaume mwenye ndoto huhitaji mwanamke mwenye maono. Na nimebarikiwa mwanamke ambaye kwa miaka 15 amekuwa akinipa sapoti isiyoyumba.
IMG_3362
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana 'Business card' na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
“Saira, nina shukurani nyingi kwako kwa kuwa nguzo ya familia yetu, mama wa heshima kwa watoto wetu watatu,” alisema Mo kwenye hafla hiyo.
Kwa utulivu, Mo alisema: “Baba, zawadi kubwa ambayo ulinipa katika maisha yangu ni muda wako, na kwa hilo nitakuwa mwenye deni la shukurani kwako siku zote za maisha yangu.”
Mo ambaye moyo wake wa binadamu ulimfanya awanie uwakilishi Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi hiyo na hivyo kuwawakilisha wanasingida kuanzia 2005 na 2015 amesema maisha ni changamoto kubwa inayobadilishwa kwa utumishi wenye nia ya dhati kwa umma.
Alisema alipowania uwakilishi alikuwa na sababu: “Nilikuwa na umri wa miaka 24, nilikwenda Singida kutoa heshima kwenye kaburi la marehemu babu yangu. Sikuwa nimefika huko tangu nilipoondoka nikiwa na umri wa miaka mitatu.
“Nilipokuwa njiani, nilimuona mzee akiwa na maji yenye rangi ya njano, machafu ambayo aliyatumia kwa kunywa. Nilishangaa, maana hali ile sikuwahi kufikiri kama ipo vile. Kipindi hicho nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani.”
Mo anasema kuwa aliingiwa na hisia kutaka kujua nini hasa alichokuwa anahitajika kufanya, alimfuata yule mzee aliyekuwa na maji yale, alipozungumza naye, aliwazungukia watu wengine na kuridhika kuwa ile ndiyo hali halisi, hapo ndipo fikra ya kwa nini agombee ubunge ilipoanzia.
Anasema kuwa baada ya kujiridhisha hivyo, alirudi kwa mzee wa kwanza, alizungumza naye na kumuuliza ni kwa nini shida ile ilikuwa haizungumzwi kwa upana katika mamlaka husika.
IMG_3434
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania.
 “Nilipojitambulisha yule mzee alisema anamkumbuka babu yangu, kisha akanishauri nigombee ubunge, alinisisitiza mno ili nisaidie kuondoa lile tatizo la watu wa Singida kunywa maji machafu,” alisema Mo.
Anaeleza kuwa alipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, alilifikiria tatizo hilo kwa mapana zaidi, akalifanyia utafiti na kubaini kwamba katika kila watu 10, watatu walikuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayosababishwa na maji machafu.
Anaendelea kusema kuwa aligundua kuwa Singida kulikuwa na tatizo kali la maji safi na salama. Anasema kuwa alibaini uwepo wa tatizo la elimu kuhusu matatizo ya maji.
Jambo lingine ambalo anasema aliligundua ni uwepo wa tatizo la huduma za afya. “Niliwafikiria watoto wangu, jinsi ninavyowapenda, na namna ambavyo kila mzazi anavyompenda mwanaye. Nilipingana na hali kuwa watoto wa Uingereza na Marekani wamependelewa zaidi. Maisha ni sawa bila kujali chochote,” anasema Mo.
IMG_3359
Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania uliombatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo.
“Niliona lazima nitimize wajibu wangu. Kutimiza malengo yangu ya kusaidia jamii, kufanikiwa katika biashara. Mambo hayo mawili hisani na biashara nimeyaweka pamoja na ndiyo maana nimefika hapa leo, tunajivunia sana kuitwa METL nembo ya Watu. Katika miaka yangu 10 kama mbunge, nimefanya mabadiliko mengi. Nilikuwa na sababu ya kupata mkopo nafuu wa dola milioni 35, ambao ulisababisha kuwekwa kwa miundombinu ya maji safi na salama Manispaa ya Singida.
“Niliitumia MeTL, tuliweza kudhamini shughuli nyingi za maendeleo ya kijamii. Kuhusu elimu, nilifanikisha kujenga shule 15, zikawa 17, kabla ya hapo tulikuwa na shule mbili tu. “Kuhusu huduma za afya, hapa nimshukuru mke wangu kwa jitihada zake. Alikuwa Mwenyekiti wa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo imekuwa ikisaidia watu wengi, hasa watoto dhidi ya maradhi ya saratani.”
IMG_3469
Burudani mbalimbali zikiendelea ukumbini hapo.
IMG_3548
Mkurugenzi Mtendaji wa Jarida la Forbes Afrika, Sid Wahi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa. Kulia ni Head of Events wa ABN Productions, Alexander Leibner.
DSC_4663
Mwanzilishi na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili kushoto)  akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia) tuzo ya Heshima Barani Afrika "2015 Forbes Africa Person of the Year"  iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).
IMG_3780
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
IMG_3776
IMG_3825
MO akiteta jambo na Mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Arunma Oteh (kulia) ambaye walikuwa pamoja kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo ambapo pia alimpongeza sana.
IMG_3849
Pichani juu na chini MO akiendelea kupongezwa na wadau mbalimbali walioalikwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3866
IMG_3875
Pongezi kwa MO zikiendelea kutolewa.
IMG_3889
IMG_3857
MO katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ambao ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.
IMG_3940
MO katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
IMG_3925
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika.
IMG_3911
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ya Afrika Kusini wakipozi kwenye 'Red Carpet'.
UNATAKA KUPATA HABARI NA BURUDANI FASTA BILA USUMBUFU ? BONYEZA HAPA

COMMENTS

Name

2014 Fifa World Cup 2baba 2face 50 Cent A.K.A A.Y Abbas Maziku Abdu Bonge Abdu Kiba Abela Music Abraham Poincheval ACT Adam Juma Adam Kuambiana Adam Mchomvu Adele adhabu Advert Afande Sele Africa African Blogger Awards African Celebs African News AFRIMA afrimama awards AFRIMMA Afya Afya Ya Mama Diamond Afya Ya Mapenzi Agatha Atiti Agnes Masogange Agness Masogange AIBU Aika AINEA Air Tanzania Airport Ajabu Ajali Ajira Aki Akon Akothee Al Shabaab Albino Album Cover Alice Kella Alikiba Aliko Dangote Ally Rehmtulah Amanda Poshy Amatus Liyumba Amazing Amber Lulu Amber rose Amina Sanani Amini AMVCA AWARDS 2014 Android Angelina Jolie Anniversary Apple Arianna Angel Arsenal Arusha Asha Baraka Aslay AT Audio August Alsina Augustine Mahiga Augustino Mrema Aunt Ezekiel Aunt Lulu Australia Avril Awards B.O.B B12 BAB J BABA DIAMOND BABA KANUMBA Babu Seya babu tale babu wa loliondo Baby Madaha BabyBoy Mapozy baeuty Banana Zoro banj Banky W Baraka Da Prince Baraka The Prince Barcelona Barnaba barua nzito Batuli BBA BBC Beef behind the scene Beka Ibrozama beki tatu Bella Belle 9 Ben Pol Benjamin Mkapa Benzema Best Nasso BET BET Awards BET Hip Hop Awards Betty Kyallo Beyonce Beyonce Knowle Biashara Bien Baraza Bifu BIG BROTHER Big Brother Hotshots Bikira Wa Kisukuma Bill Clinton Bill Nass Biography BirdMan Birthday Blac Jizzle Black Chyna Blue Ivy Bob Juniour Bob Marley Bobbi Kristina Brown Bobic Bondia Bonge la nyau Bongo Celebs Bongo Flava Bongo Fleva Bongo Movie Bongo Movies Bongo Swaggz Shindano Bongo Swaggz Tv Bongo Videos BongoSwaggz BongoSwaggz Play Store BOT Bow Wow Brad Pitt Brasil Breaking News Brown Mauzo Brown Punch (Bavoo) Brussels BS BSS BUNGE LA KATIBA. BUNGENI BURUDANI Bushoke Business C Pwaa C.E.O C9 Calisah Camon C9 CANCER Cannical Captain Komba Cars Carter V CashTime cazuza bon scott CCM Celebrities Celebrities Gossip Celebs CHADEMA Chagga Barbie Chagga Barbie na Zari The Boss Lady Changes Channel O Chege Cheka Chelsea Chibu Wayaya Chibu West Chicharito Chid Benz Chidi Mapenzi Chidinma Chin Bees China Chris Brown Chriss Brown christian bella Christian Ronaldo christina hewitt Chuchu Hans Ciara Clouds Fm Clouds Media Club La Liga Coke Studio Collabo Colonel Mustafa Comedy Coming Soon Corazon Kwamboka Coyo Mc Crimes Cristiano Ronaldo CSEE 2013 RESULTS Cyril Kamikaze d D banj d'banj D’banj damian soul Dance Dar es salaam darasa darasa la mapenzi darassa Dassy Amazing David Moyes Davido Davis mosha DAVIS MWAMUNYANGE Dawa Dawa Vidonda Vya Tumbo Dayna Death Decent Boy deddy Diamond Diamond na Zari Diamond Platnumz Diamond Platnumz Vs Davido Diana Kimaro DIDA Dillish Dipper Diva Diva Loveness Love divathebawse Dj Choka Dj D-Ommy Dj Fetty Dj Khaled Dj Sinyorita Dj Young Guru Dk. Vincet Mashinji Dkt. Asha-Rose Migiro Dog dogo janja Dogo Mfaume Don Jazzy Don Tach Donald Trump Doris Mollel Foundation Dr Cheni DR JOSE CHAMELEONE Dr. Dre Dr. John Pombe Magufuli Dr. Mwaka Dr. Slaa Drake Drinks DRM DSTv Dude DUDU BAYA dullayo Dully Sykes Dunga Duterte Dwayne Johnson EATV Awards Eddy Kenzo Education Edward Lowasa Elimu Elizabeth Michael Eminem Emmanuel Adebayor Emmanuel Mbasha Enos Olik Entertainment EPL Eric Omondi ESCROW Esma Platnumz Ethiopia Etihad Europe Evander Holyfield Events Exclusive Ezden Ezekiel Wenje Facebook Fadhili Awadh Fahyma Faiza FALLY IPUPA Fashion Fast & Furious Fast &Furious 7 Fast And Furious 8 Ferouz Fetty Feza Kessy Fid Q Fiesta 2013 FIESTA 2014 FIFA Filikunjombe First Godfrey Flaviana Matata Flora Mbasha Florah Mvungi Floyd Mayweather FM Academia Footballer Forads Forbes Fred Swagg Freeman Mbowe freemason freemason tanzania French Montana FUMANIZI Fuse ODG Future JNL G Nako G-Nako GABO ZIGAMBA Gadner Habash Galaxy Glass Gari Inauzwa gari mpya Geez Mabovu Gelly wa Rhymes GENEVIEVE Gentriez ghana Ghetto Kids Gift Gigy Money Girls global publisher Gmail Gnako Godbless Lema Godfather Godzilla Goodluck Gozbert Google Google Glass Gospel Gossip Grace Msale gwajima H BABA Habari Hakeem 5 Halima Kimwana Halima Mdee halimaty msodoki HAMISA MOBETO Hanscana Happiness Watimanywa Haristot Shungu Harmonize Harusi Hasheem Thabit Health Hemedi Hemedi Suleiman "PHD" Hillary Clinton Hip Hop HiPipo Awards HollyWood Homa La Jiji Hot In Town hot photo How To How to Love HTC Huddah HUSNA HUSNA MAULID Hussein Machozi Ian Ferrao Ice Prince Idris Sultan Imetosha Imetosha Campaign India Injili Instagram Interview iPhone iPhone 6 News iPhone 7 Irene Paul Irene Uwoya Iringa Isabela Issaya Mwita Charles Ivan Don Iyanya Izzo Business jack Cliff Jack Pemba Jackline Wolper jaguar Jah Prayzah Jakaya Mrisho Kikwete Jambo Squad Jamii January Makamba jaraja kubomoka jason deruLo jason deruro Jay C Jay Z JB Jini Jini Kabula Joh Makini Johari JOHN CENA John Legend john lennon John Mnyika John Woka Johnnie Walker Jokate jomo kenyata jordin sparcks Jose Mourinho Joseph Mbilinyi Joseph Msukuma Joti Joyheart Events JPEG Jude Okoye Juma Kaseja Juma Nature Jussie Smollett Justin Beiber Justin Bieber Jux K Lyamo K-LYN K.O K’naan kajala Kala Jeremiah Kalakala Kamikaze Kanga Moko Kanumba KANUMBA DAY Kanye West Karrueche Kassim Majaliwa Kayumba KCEE KCMC keisha Kelly Rowland Kenya kenya celebs Kesi Kevin-Prince Boateng Khadija Kopa Kiba Square Kidoa Kifo kigamboni Kigwangalla kikwete Kili Home Kilimanjaro Kilimanjaro Premium Lager Kim Kardashian Kimbunga Mchawi King Crazy GK King Kaka King Lawrence king majuto Kingunge Kitale Kizz Kiduku Klyn Koffi Olomide KOREA KR Mullah KTMA Kubenea kujinyonga kujiua Kupatwa Kwa Jua Kush Tracey Kutongoza Kylie Jenner LAANA LADY GAGA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lagos Laveda Le Mutuz leo Leo Mysterio Life Style Lij Michael LIL DRAINO lil kim Lil Wayne Linah Linex Lira Galore Live Updates Liverpool LOL Lola-Rae Lord Eyes Lost Airplane Love Love And Relationship Love Matters Love Story Love Tips Love Zone Lucci Luis Figo Luis Munana Lulu Lulu La Diva Lundenga Lupita Nyong'o Lynn M-Pawa M-Pesa m-rap MAAJABU Maalim Seif Sharif Hamad Mabeste MABOMU Mabruki Madam Rita Madawa ya Kulevya madee mademu Madhara Ya Mafikizolo MAFURIKO YA MAJI mafuriko ya mvua Magari Mazuri magazeti maimartha jesse Mainda Maisha Majanga Majay Makala makalio Makamba makavu live Make Love Makomando Malaika Malawi Malaysia malaysia airlines Malia Obama Malkiz MAMA DIAMOND MAMA KANUMBA Mama Lulu mama sharo milioneo Mama Wema Man Fongo Man u Man Utd Manchester City Manecky Mange Kimambi mangwea Manji Manny Pacquiao Mapenzi Maphorisa marilyn monroe Mario Balotelli Mark Zuckerberg Markson Beauty Products Marlaw Maromboso martin kadinda Masanja mkandamizaj Mashabiki masoud kipanya Mastaa Mastaa Bongo Master J matako bandia matokeo Matokeo Form Six Matokeo Kidato Cha Nne 2013 Matokeo Kidato Cha Nne 2015 Matonya MATUKIO Maua Maua Sama mauaji maximo MAYA Mayunga MB Dog mbagala Mbeya Mbinu Za Mapenzi MBWA WA WEMA Mc Dulla Mch. Christopher Mtikila Mechi Medicine Meek Mill Mekstar Melania Trump Menina Meninah Mesen Selekta Messenger Messi Mgomo Mh Job ndugai Mi-Casa Micah Boy Michael Jackson Michelle Obama Michepuko Michezo Mike Scotter Mike Tyson milipuko Millard Ayo Millen Magese Mimba Mirror Miss Bongo Movie Miss Bongo Muvi Miss Kilimanjaro 2016 Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 Miss KK Miss Rwanda Miss Tanzania Miss Tanzania 2014 Miss Uganda Miss World misukule Mkasa Mkasi mke wa sugu Mkubwa Na Wanawe Mkude Simba Mlela Mlimani City Mo Dewji mo music Mobile App Model Classic Models moe musa monalisa morogoro Mose Iyobo Moshi Movie Moyo Tara Flavour mpira Mr Blue Mr Flavour Mr Nice Mrema Mrembo Mrembo wa Wiki mrisho mpoto Msaga Sumu Msami Msiba Msigwa Mswaki MTANGAZAJI TIMES FM Mtoto Mtoto Wa Diamond mtoto wa nay wa mitego MTV MTV EMA MTV MAMA MUAJI Mubenga Muchoma Mugabe Muhammad Ali Multichoice Africa Muna Music MUSIC Mustapha Jaffer Sabodo Mwana FA Mwanafunzi Mwanamke MWANZA Mwasiti MZEE GURUMO Mzee Wa Upako Mzee Yussuf Mzee Yusuf Mziiki mzungu kichaa Nafca Nahreel Naj Nakaaya Nald Clever Nameless Nana Kwaku Bonsam NANDO Nape Nnauye Nash MC Nasibu Abdul Juma navy kenzo Nay Wamitego Nazizi Ndege Kupotea ndege ya malaysia Ndikumana Ndoa NEC NECTA Nedy Music Nelly Kamwelu Nelson Mandela Nemo New Blog New Maisha Club new movie New Product new ride New Track New Video News Ney Wa Mitego Neyo Ngasa ngono ya mdomo nguo za kubana Ngwea Nick Wa BongoSwaggz Nicki Minaj Nickson Lema niger celebs Nigeria Nikki Mbishi Nikki wa II Nikki Wa Pili Nisha Nisher Nisher Bye Nisher Entertainment Nissan Note Niva Nixl Carter Nokia Nonini Nora Nuh Mziwanda Nuhu Mziwanda nyerere Nyu Kid Obama Ochu Sheggy Octopizzo Odama Ojwang Olamide Ombeni Sefue Ommy Dimpoz Omotola Omotola Jalade Ekeinde One The Incredible Oprah Winfrey Ordinareh Bingwa Oscar Awards ostaz juma Ousmane Dembele P Diddy P Square P The Mc Pah One pakistan Pam D Pancho Chineke Panya Road Papa Francis Papa Wemba Papaa Masai Papi Kocha Paradise parliament Party Patcho Mwamba Patoranking Paul Kagame Paul Makonda Paul Okoye Paul Pogba Paul Walker Paula Penny Perfect Internet Peter Msechu Peter Okoye Petit Man Photo Photo Of The Day Picha picha za uchi picha chafu picha kli Picha Program Picha Ya Picha za mastaa Picha Za Matukio Picture pingu Pipi Pitbull PNC Political Issues Politics pombe Prezzo Princess Tiffah Privacy Priyanka Chopra Producer Prof. Ibrahaim Lipumba Profesa Jay Promo Promotion Q Chief Queen Darleen Queen Darling Quick Rocker R.I.P Raila Odinga rally Rama Dee Rammy Galis Range Rover Sport Raph Tz Ray Ray C Ray Vanny Raymond Rayuu RayVanny Read Madrid Real Madrid Recho Reekado Banks Regina Lowassa Reginald Mengi Rehab Relationship REMIX Rich Mavoko Rich People Richard BBA 2007 Richie Rick Ross Ridhiwani Kikwete Rihanna Rijo Voive RISPER Riyama Robin Thicke Rolene Strauss roma mkatoliki Romeo Romy Jons Rosa Ree Rose Muhando Rose Ndauka Rossie M Rostam Aziz Ruby RunTown Rwanda Sabby Sad News Saed Kubenea Safari Lager said fella Saint West Salam Tmk Salama Condom salama jabir Salamu Tmk Salha Israel Sallam Sk Salman Khan Salomon Kalou Sam Misago samaki wa ajabu Samantha Samatta SamBoy Samsung Samsung Galaxy S5 samweli sita Sarkodie Sasha Obama Sauda Mwilima Sauti Base Sauti Sol SBL sean kingston Secky Seki Selena Gomez Seline Selling Child Senga Serengeti Sergio Agguero Sergio Aguero Serikali Sexy Seyi Shay Shaa Shababi Shamsa Ford SHAMSA SORD Share SHARLEEN Sharo Millionea Sheddy Clever Shein Sherry Zuu Sheta Shetta Shevchenko Shilole Shocking News Sholo Mwamba Show Siasa SIKU KUU YA WAJINGA Simba Simulizi Sintah Siri Ya Mtungi Sitti Mtemvu Siwema Skendo snake bit Snoop Dogg Snura SOAP soccer Social Matters Social Networks SOKO LA KARUME Solution Somalia Somo Songa Sonko Sony South Africa spark Sport News Stamina Stan Bakora Stand United Stanna Stereo Steve Nyerere Steve RnB Steven Nyerere Stone Bone Stori Stori za Bongo Story Lounge suarez subaru Subaru Legacy Sudan SUGU Sumaye Super Nyota 2013 Swahili Jokes Swahili Music T-Pain T.I tahadhari Tajiri Talents Tamthilia tancredo neves tanesco Tangazo Tania tanz TANZANIA Tanzania Film Tanzania Music Tanzania News Tanzania One Tanzanian Tanzanian Actress Tanzanian music Tanzanian Rapper Tayo Folarin TB Joshua TBC Fm TBT TCRA TCU Teachers Technology Tecno Tekno Miles temba Tembo Tetesi TFF Thado The Game The Industry The Next Billionea Thea THT Tiara TID Tiffah Tigo Tiko Timbulo Times Fm Tinashe tip top connection Tiwa Savage tmk Togo Tottenham Hotspur Touch Phone TRA Trace TV trafiki trey songz Trick And Tips Tricks Tros Machine Trubadour George True Story Trust Trust Life TSH to USD Tuddy Thomas Tumaini University Tunda Tunda Man Tundu Lissu Tunisia Tupac Tusker Tuzo Tuzo za watu 2014 Twenty Percent Twerk Video Twitter Tyga U Heard ubakaji UCHAGUZI 2015 Uchawi Uchumi Supermarket ud Udaku Udaku Bongo Udaku Wa Bongo UDOM Uganda ugomvi ugomvi wa wema na kajala Uhuru Uhuru Kenyatta Uhusiano ukatili UKAWA Ukwa Umalaya UNESCO University News Unyama Urembo USA USA Celebs usagaji Usain Bolt Ushauri Usher Raymond Ushoga uswahilini uswazi Utabiri utajiri Utamu Vai Wa Ukweli Valentine Valentine's Day Van Persie Van Vicker vanessa chettle Vanessa Mdee Vannesa Mdee Venezuela VENGU VERA SIDIKA Vicent Kigosi vicent nyerere Vichekesho victoria kimani Video video queen Videos Vin Diesel visa vya mapenzi Vituko Vj Adams VJ Penny Vodacom vurugu Wahu WAJE Wale Walter Chilambo Wanawake Warning wasanii Wasira wastara Wayne Rooney wazungu WCB Wasafi Wedding Wedding Tanzania Weight Loss Welu Sengo WEMA Wema Sepetu wema sepetu alia wema sepetu kuzaa wema sepetu na ugumba Westgate Weusi Whatsapp Wildad William Bugeme Windhoek Beer Wise De Africa Wise One Witchcraft Witnesz wiz khalifa wizi Wizkid Wonder World News World Record Yamoto Band Yanga Yasinta Ycee Yemi Alade yesu bandia YMCMB Young D Young Dee: Situmii Madawa ya Kulevya ila Napiga Mtungi Kwa Sana Young Killer Young Money Yoweri Museveni yuzo mkali yvone chakachaka Z Anto z-anto zamaradi mketema Zanzibar Zari Zari All White Party Zari The Boss Lady Zimbabwe Zitto Aama Chama zitto kabwe Zitto Kabwe ACT Zlatan Ibrahimovic Zuhura Gora Zuleha Zuzu
false
ltr
item
BongoSwaggz.Com : MO DEWJI APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA
MO DEWJI APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA
https://ci3.googleusercontent.com/proxy/yxS5zGKMj5b2rvRqqsFNqpf-9u5JCCN44hnKumf4vTbEtFFZSWbwiHGINZaACqEaPj6r_BDoC-iVlxLIq_DcfcJVEjQWdNmPLdpjb7D2-fYRsA=s0-d-e1-ft#http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/11/IMG_3351.jpg
https://ci3.googleusercontent.com/proxy/yxS5zGKMj5b2rvRqqsFNqpf-9u5JCCN44hnKumf4vTbEtFFZSWbwiHGINZaACqEaPj6r_BDoC-iVlxLIq_DcfcJVEjQWdNmPLdpjb7D2-fYRsA=s72-c-d-e1-ft#http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/11/IMG_3351.jpg
BongoSwaggz.Com
http://www.bongoswaggz.com/2015/11/mo-dewji-apata-tuzo-nyingine.html
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/2015/11/mo-dewji-apata-tuzo-nyingine.html
true
371784233821042440
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy