Advert

Breaking News

Alikiba Anahisi Kafanyiwa Mchezo Mchafu Kwenye Tuzo za AFRIMA Baada ya Kukosa Zote Alizokuwa Ametajwa

Muimbaji huyo alikuwa ametajwa kuwania vipengele vinne kwenye tuzo za Afrima zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria.

Kiba alitajwa kuwania Best Male Artist East Africa, Artist of The Year, Song of the Year na Song Writer Of The Year In Africa. Tuzo tatu kati ya hizi zimechukuliwa na Diamond waliyekuwa wametajwa pamoja.

Kupitia post aliyoweka kwenye Instagram, Alikiba amedai kuwa anaamini ‘kuna watu’ wanaotumia fedha kuhakikisha anakosa tuzo.

Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #kingkiba,” ameandika Alikiba.

Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa muziki.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

1 comment

nzundah said...

Check out this link http://theyouthjob.com/?ref=7875

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.