Exclusive: Mastaa 15 wenye nguvu zaidi Afrika Mashariki – 2015

Kiwanda cha burudani katika eneo la Afrika Mashariki kimeendelea kuchangamka zaidi kadri miaka inavyokwenda. Kwa sasa hakuna ubishi kuwa Afr...

Kiwanda cha burudani katika eneo la Afrika Mashariki kimeendelea kuchangamka zaidi kadri miaka inavyokwenda. Kwa sasa hakuna ubishi kuwa Afrika Mashariki inatoa upinzani wa kueleweka kwa nchi za Afrika Magharibi na Kusini ambazo kwa miaka mingi zimeendelea kuwa kitovu cha burudani barani Afrika.
1555
Hii ni orodha ya Bongo5, ya mastaa 15 walio na nguvu zaidi mwaka 2015, kutoka nchini za Afrika Mashariki. Baadhi ya mastaa hawa sio mastaa tu wa Afrika Mashariki ama barani Afrika pekee, bali kwa sasa wanajulikana dunia nzima.

1. Lupita Nyong’o – Kenya

Lupita
Lupita Nyong’o ni jina maarufu mno duniani kwa sasa. Umaarufu wake kwa Afrika Mashariki ulianzia kwenye tamthilia ya mwaka 2009, Shuga. Umaarufu wake duniani, ulitokana na kuigiza filamu iliyoshinda tuzo za Oscar, ’12 Years A Slave.’
Kwenye filamu hiyo aliigiza kama Patsey, mtumwa wa kike aliyejikuta akipata shida kubwa kwa kazi ngumu za mashambani. Uhusika wake kwenye filamu hiyo ulimfanya mwaka jana ashinde kipengele cha muigizaji msaidizi wa kike bora kwenye tuzo za Oscar. Ushindi huo ulimfanya kuwa muigizaji wa kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda tuzo hizo za thamani.
Pia aliigiza kama mhudumu wa ndege kwenye filamu ya action ya mwaka jana, Non-Stop akiwa na Liam Neeson na Julianne Moore. Mwaka huu ameigiza filamu iitwayo Queen of Katwe na Star Wars Episode VII: The Force Awakens.
Umaarufu wake ulimpa deals zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa kisura wa kampeni ya Miu Miu akiwa na walimbwende wengine, Elizabeth Olsen, Elle Fanning na Bella Heathcote. Alionekana kwenye majarida makubwa ya fashion duniani yakiwemo Dazed & Confused huku akiwa mwanamke wa pili wa Afrika na wa nane mweusi, kukava jarida la Vogue.
April mwaka jana, jarida la People lilimtaja Lupita kama mwanamke mrembo zaidi duniani katika issue yake ya ’50 Most Beautiful.’
2015, Nyong’o alikava jarida la Lucky, Harper’s Baazar’s (UK) na MujerHoy la Hispania.
Wiki hii Lupita amerejea nchini Kenya ambako alitangazwa pia kuwa balozi wa taasisi ya WildAid inayojihusisha na kampeni dhidi ya ujangili hususan wa tembo.
2. Diamond Platnumz – Tanzania
Diamond
Diamond amekuwa si jina maarufu Afrika Mashariki peke yake na sasa miongoni mwa wasanii wakubwa kabisa barani Afrika. Mwaka huu peke yake ametengeneza nyimbo kubwa na collabo na wasanii maarufu Afrika zilizoshika charts kwenye vituo vya redio na runinga vikubwa. March 27 aliachia video ya wimbo wake wa Mduara, ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa ambao haukuishia kufanya vyema Afrika Mashariki peke yake, bali Afrika nzima. Hadi sasa video yake imeangaliwa kwenye mtandao wa Youtube kwa zaidi ya mara milioni 2.7.
Collabo yake kubwa kwa sasa ni ‘Nana’ aliyomshirikisha Flavour ambayo licha ya kushika chart za redio na TV Afrika ikiwa ni pamoja na kuwa namba moja kwenye kituo cha Trace TV, video ya wimbo huo ni miongoni mwa zile zinazoangaliwa kwa kasi zaidi kwenye Youtube barani Afrika, ikiwa na views zaidi ya milioni 2.1 tangu iwekwe May 29. Bila kusahau mwaka jana alishirikishwa kwenye nyimbo zilizohit za wasanii wa Nigeria, likiwemo kundi la Bracket na Waje.
Hivi karibuni tu video mbili za nyimbo alizoshirikishwa na wasanii wakubwa wa Nigeria zimetoka – Nakupenda aliyoshirikishwa na Iyanya na Love Boat aliyoshirikishwa KCEE.
Pia aliingia studio kurekodi wimbo aliorekodi na msanii wa Afrika Kusini, Donald. June 13 alishinda tuzo mbili kwenye KTMA 2015. Mwaka huu ametajwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo za MTV MAMA na ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza July 18 kwenye utoaji wa tuzo hizo, Durban, SA. January mwaka huu staa huyo alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo za Glo CAF jijini Lagos, Nigeria.
3. Wema Sepetu – Tanzania
wema
Umaarufu wa Wema Sepetu na kuendelea kutengeneza vichwa vya habari Afrika Mashariki, unaendelea kuwepo kutokana na uhusiano wake uliokufa na Diamond miongoni mwa mambo mengine. Wema bado ameendelea kuwa staa wa kike mwenye mashabiki na ushawishi mkubwa nchini Tanzania.
Mwaka huu alishinda tuzo ya muigizaji wa filamu wa kike anayependwa zaidi kwenye Tuzo za Watu. Alisafiri hadi nchini Ghana kwenye kutengeneza filamu na muigizaji wa maarufu wa huko, Van Vicker, ambayo inatarajiwa  kutoka mwishoni mwa mwaka huu. Ameendelea kutengenezwa vichwa vya habari kutokana na kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia CCM, mkoani Singida. Kama mambo yakimwendea vyema, huenda jina lake mwaka huu likabadilika na kuwa Mheshimiwa Wema Sepetu.

4. Zari the Bosslady – Uganda

11377544_1677216072511891_1896615064_n
Kabla ya kukutana na Diamond, Zari The Bosslady alikuwa maarufu nchini Uganda. Alijulikana kwa urembo wake na utajiri mkubwa aliokuwa nao kupitia aliyekuwa mumewe, Ivan. Alifahamika kama mwanamke anayemiliki magari ya kifahari, mijengo na biashara kubwa. Umaarufu wake umekuja kukua zaidi baada ya kukutana na Diamond Platnumz na kuanzisha uhusiano ambao sasa umewafanya kuwa couple yenye nguvu zaidi Afrika Mashariki. Kwa sasa wawili hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Mtoto huyo bila shaka ana nafasi kubwa ya kuwa mtoto maarufu zaidi Afrika Mashariki.
5. Vanessa Mdee – Tanzania
11692681_10153475410864600_8788807616217154510_n
Vanessa anafahamika kama msanii wa kike kutoka Afrika Mashariki anayejituma zaidi kuliko wote. Mwaka huu ameshiriki kwenye kampeni nyingi za kimataifa. Alishiriki kwenye kampeni ya One Organisation ambapo aliungana na wasanii wengine wa Afrika kuimba wimbo uitwao Strong Girl. Pia aliungana na mastaa wakiwemo Lupita Nyong’o, Hasheem Thabeet, Jacqueline Ntuyabaliwe na Alikiba kama mabalozi wa WildAid na kampeni dhidi ya mauaji ya tembo.
Mwaka huu ametajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa kike kwenye tuzo za MTV MAMA. Wimbo wake ‘Nobody But Me’ aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O, ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri Afrika kwa sasa. Mwezi ujao ataonekana kwenye jarida maarufu la Marekani la Essence kwenye toleo lake la dunia (global issue). Ni balozi wa Samsung na Crown Paints.
6. Millen Magese – Tanzania
millen-magese-x-joice-jacobs_1-2
Happiness Millen Magese @ladivamillen amejipatia umaarufu mkubwa mwaka huu kutokana na kuwa balozi kwenye kampeni aliyoanzisha mwenyewe ya tatizo la Endometriosis ambalo limepelelekea afanyiwe upasuaji kwa takriban mara 13 na kumfanya awe mgumba. Millen ameanzisha kampeni ya kukuza uelewa wa ugonjwa huo na kuwataka wanawake wenye tatizo hilo kutooana aibu kujitokeza kuomba msaada lakini pia kuwataka wanaume wenye watu wao wa karibu walio na tatizo hilo kuwavumilia. Kutokana na jitihada hizo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kusaidia watu wasiojiweza, June mwaka huu alitunukiwa tuzo ya Global Good ya BET Awards.

7. Eddy Kenzo – Uganda

photo2-ddy
Jina la Edrisa Musuuza maarufu kama Eddy Kenzo halikuwa maarufu sana kwa Tanzania na Kenya kabla ya June mwaka huu kushinda tuzo ya BET ((Best Viewers’ Choice International Act). Anahamika zaidi kwa hit yake Sitya Loss. Wimbo huu ulifahamika duniani kupitia video ya Youtube ya vijana wa mtaani waliokuwa wakicheza wimbo huu. Video hii ilikuwa maarufu kiasi cha kuwepo na ombi (petition) ili vijana hao waweze kuhojiwa kwenye The Ellen DeGeneres Show. Hadi sasa video hiyo ina views zaidi ya milioni 11. 9.
Kenzo ameshatumbuiza kwenye majiji 15 ya Marekani. Ametembelea na kutumbuiza kwenye majiji kibao duniani. Alitumbuiza kwenye fainali za mataifa ya Afrika.
8. Sauti Sol – Kenya
sauti-sol-press
Bien-Aimé Baraza, Willis Chimano, Delvin Mudigi na mpiga gitaa wao Polycarp Otieno ndio wanaunda kundi la Sauti Sol.
Mwaka huu walitajwa kuwania tuzo za BET japo hawakufanikiwa kushinda. June 13, walichukua tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kwenye KTMA 2015 na wimbo wao uliokuwa anthem ya Afrika Mashariki, ‘Sura Yako.’ Mwaka huu wanawania kipengele cha kundi bora kwenye tuzo za MTV MAMA. Kwa sasa wapo kwenye ziara ndefu nchini Marekani.
9. Alikiba – Tanzania
11328304_734078546715202_847618383_n
King Kiba kama anavyojiita, aliufungua mwaka 2015 kwa kishindo na hakuna anayeweza kubisha kuwa jamaa huyu ana ushawishi mkubwa nchini Tanzania. Milango yake ya umaarufu nje ya Tanzania imefunguka tena mwaka huu baada ya kuwa kimya kwa takriban miaka mitatu.
Video ya wimbo wake ‘Chekecha Cheketua’ ilichezwa kwa mara ya kwanza kwenye kituo cha Trace Urban na kuendelea kupata rotation ya mara tano kwa siku. Mwaka huu Alikiba alishinda tuzo ya muimbaji wa kiume anayependwa kwenye Tuzo za Watu na kushinda tuzo takriban sita kwenye KTMA 2015.
Mwaka huu pia ameungana na wasanii wengine wa Afrika kwenye msimu wa tatu wa kipindi cha Coke Studio Afrika huku akitengeneza timu na msanii wa Kenya, Victoria Kimani. Pia aliungana na Lupita Nyong’o, Vanessa Mdee na K-Lynn kama balozi wa WildAid katika kampeni dhidi ya mauaji ya tembo.
10. Idris Sultan – Tanzania
11373827_869378469836710_322892383_n
Ushindi wa $300,000 wa shindano la Big Brother Africa mwaka jana, umemfanya Idris kuwa miongoni mwa mastaa wakubwa Afrika kwa sasa. Japokuwa hajaanza kufanya miradi mingi, ukubwa wa shindano hilo umeendelea kuliweka jina lake kwenye headlines. Lakini pia uhusiano wake na mshiriki mwenzie wa shindano hilo, Samantha umewafanya wawili hao kuokota headlines za hapa na pale kwenye vyombo vya habari vya Afrika. Idris anafahamika kwa vituko vyake na huenda akawa na nafasi kubwa ya kuingiza fedha nyingi kupitia kipaji hicho miongoni mwa vingi alivyo navyo.
11. Jaguar – Kenya
jaguar
Jaguar alitengeneza headlines mwaka huu kwa mambo mengi ikiwemo kurushiana maneno na msanii wa Nigeria, Iyanya aliyemshirikisha kwenye remix ya wimbo wake ‘One Centimeter. Ugomvi ulitokana na shutuma ya Jaguar dhidi ya msanii huyo kuwa alikuwa akimletea mapozi wakati wa mipango ya kufanya video ya wimbo huo.
Iyanya alijibu kwa kumwelezea msanii huyo kama ‘asiye serious’ na muziki.
Pamoja na kufanya muziki, Jaguar ameendelea kuandikwa zaidi kutokana na juhudi zake za kuwainua watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na kazi zake kwenye taasisi za serikali ikiwemo NACADA. Hivi karibuni alijitolea kumsomesha kijana mwenye umri wa miaka 16 aliyeruka uzio wa ikulu ya Kenya ili kwenda kukutana na Rais Uhuru Kenyatta ili amsaidie kumlipia hela ya studio kurekodi muziki.
“Promised to look for him after jumping statehouse and i have found him . . ..he is 16yrs and best i can do for now is take him to school…he dropped form 1 coz of lack of fees……he has a kikuyu song titled Jubireeeee bt muziki baadaye,” aliandika Jaguar kwenye Instagram.
12. Jose Chameleone – Uganda
11083913_785893748154344_8571962429917640031_n
Chameleone ni miongoni mwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaoingiza fedha nyingi zaidi kupitia show nyingi za ndani na za kimataifa. Mwaka huu ameingia kwenye tuzo za MTV MAMA kwenye kipengele cha Evolution Award. Pia naye ameungana na wasanii wengine wa Afrika kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio Africa. Video ya wimbo wake ‘Wale Wale’ ilifanya vizuri barani Afrika ikiwa ni pamoja na kushika chart za muziki wa bara hilo kwenye kituo cha runinga cha Trace Urban.

13. Victoria Kimani – Kenya

HouseOfMaliq-Magazine-2015-Victoria-Kimani-Cover-February-Edition-Tiannah-Styling-22288833-683x1024
Victoria Kimani aliungana na Vanessa Mdee na wasanii wengine kwenye kampeni ya One kurekodi wimbo ‘Strong Girl.’ First Lady huyu wa Chocolate City ameendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Afrika ikiwa ni pamoja na mwishoni mwa mwaka uliopita kutoa hit single, ‘Show.’ Nyimbo zake zinapata rotation kubwa kwenye redio za Afrika pengine kuliko msanii yeyote wa Kenya.
Mrembo huyo wiki hii ameshinda tuzo ya ‘Most downloaded Female In Africa’ kwenye Mdundo Awards 2015 aliyokabidhiwa na Alikiba. Kimani na Alikiba wanashiriki pamoja kwenye Coke Studio Africa.
14. AY – Tanzania
AY
Mwishoni mwa mwaka uliopita, (Dec 9) na mwanzoni mwa mwaka huu (Feb), AY aliachia video za collabo za kimataifa. Ya kwanza ni wimbo wake ‘Love Me’ aliomshirikisha Sean Kingstone na Ms Trinity na ‘It’s Going Down’ aliyowashirikisha Ms Trinity na Lamyia Good. Video hizo zilishika charts kadhaa kwenye runinga za Afrika.
Alikuja kuachia hit single yake ‘Zigo’ ambayo hadi sasa imeendelea kuwa miongoni ma ngoma zinazochezwa zaidi redioni nchini Tanzania. Beat ya wimbo huo inatarajiwa kutumiwa na wasanii wengine wengi kutengeneza version zao. Wasanii walioonesha interest ya kuitumia ni pamoja na Jose Chameleone na Wizkid wa Nigeria.
AY ameendelea kuwa msanii anayeheshimika zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na mwaka huu kushiriki kama mentor kwenye shindano la Maisha Superstar. Pamoja na muziki, AY ni mjasiriamali analiyefanikiwa. Ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha TV ‘Mkasi’ kilichoshinda kwa miaka miwili mfululizo tuzo ya kipindi cha runinga kinachopendwa katika Tuzo za Watu 2015. Pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi kingine cha TV, Siaza za Siasa.

15. Bebe Cool

10922491_10153076830868313_8283993024498490227_n
Mwaka huu Bebe Cool anawania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha video bora ya mwaka. Wimbo wake ‘Love You Everyday’ umehit sana katika kipindi cha mwaka 2014/15 na video yake ndio inayowania tuzo hiyo. Bebe Cool ameendelea kuwa miongoni mwa wasanii wanaoheshimika zaidi nchini Uganda.

-bongo5 UNATAKA KUPATA HABARI NA BURUDANI FASTA BILA USUMBUFU ? BONYEZA HAPA

COMMENTS

Name

2014 Fifa World Cup 2baba 2face 50 Cent A.K.A A.Y Abbas Maziku Abdu Bonge Abdu Kiba Abela Music Abraham Poincheval ACT Adam Juma Adam Kuambiana Adam Mchomvu Adele adhabu Advert Afande Sele Africa African Blogger Awards African Celebs African News AFRIMA afrimama awards AFRIMMA Afya Afya Ya Mama Diamond Afya Ya Mapenzi Agatha Atiti Agnes Masogange Agness Masogange AIBU Aika AINEA Air Tanzania Airport Ajabu Ajali Ajira Aki Akon Akothee Al Shabaab Albino Album Cover Alice Kella Alikiba Aliko Dangote Ally Rehmtulah Amanda Poshy Amatus Liyumba Amazing Amber Lulu Amber rose Amina Sanani Amini AMVCA AWARDS 2014 Android Angelina Jolie Anniversary Apple Arianna Angel Arsenal Arusha Asha Baraka Aslay AT Audio August Alsina Augustine Mahiga Augustino Mrema Aunt Ezekiel Aunt Lulu Australia Avril Awards B.O.B B12 BAB J BABA DIAMOND BABA KANUMBA Babu Seya babu tale babu wa loliondo Baby Madaha BabyBoy Mapozy baeuty Banana Zoro banj Banky W Baraka Da Prince Baraka The Prince Barcelona Barnaba barua nzito Batuli BBA BBC Beef behind the scene Beka Ibrozama beki tatu Bella Belle 9 Ben Pol Benjamin Mkapa Benzema Best Nasso BET BET Awards BET Hip Hop Awards Betty Kyallo Beyonce Beyonce Knowle Biashara Bien Baraza Bifu BIG BROTHER Big Brother Hotshots Bikira Wa Kisukuma Bill Clinton Bill Nass Biography BirdMan Birthday Blac Jizzle Black Chyna Blue Ivy Bob Juniour Bob Marley Bobbi Kristina Brown Bobic Bondia Bonge la nyau Bongo Celebs Bongo Flava Bongo Fleva Bongo Movie Bongo Movies Bongo Swaggz Shindano Bongo Swaggz Tv Bongo Videos BongoSwaggz BongoSwaggz Play Store BOT Bow Wow Brad Pitt Brasil Breaking News Brown Mauzo Brown Punch (Bavoo) Brussels BS BSS BUNGE LA KATIBA. BUNGENI BURUDANI Bushoke Business C Pwaa C.E.O C9 Calisah Camon C9 CANCER Cannical Captain Komba Cars Carter V CashTime cazuza bon scott CCM Celebrities Celebrities Gossip Celebs CHADEMA Chagga Barbie Chagga Barbie na Zari The Boss Lady Changes Channel O Chege Cheka Chelsea Chibu Wayaya Chibu West Chicharito Chid Benz Chidi Mapenzi Chidinma Chin Bees China Chris Brown Chriss Brown christian bella Christian Ronaldo christina hewitt Chuchu Hans Ciara Clouds Fm Clouds Media Club La Liga Coke Studio Collabo Colonel Mustafa Comedy Coming Soon Corazon Kwamboka Coyo Mc Crimes Cristiano Ronaldo CSEE 2013 RESULTS Cyril Kamikaze d D banj d'banj D’banj damian soul Dance Dar es salaam darasa darasa la mapenzi darassa Dassy Amazing David Moyes Davido Davis mosha DAVIS MWAMUNYANGE Dawa Dawa Vidonda Vya Tumbo Dayna Death Decent Boy deddy Diamond Diamond na Zari Diamond Platnumz Diamond Platnumz Vs Davido Diana Kimaro DIDA Dillish Dipper Diva Diva Loveness Love divathebawse Dj Choka Dj D-Ommy Dj Fetty Dj Khaled Dj Sinyorita Dj Young Guru Dk. Vincet Mashinji Dkt. Asha-Rose Migiro Dog dogo janja Dogo Mfaume Don Jazzy Don Tach Donald Trump Doris Mollel Foundation Dr Cheni DR JOSE CHAMELEONE Dr. Dre Dr. John Pombe Magufuli Dr. Mwaka Dr. Slaa Drake Drinks DRM DSTv Dude DUDU BAYA dullayo Dully Sykes Dunga Duterte Dwayne Johnson EATV Awards Eddy Kenzo Education Edward Lowasa Elimu Elizabeth Michael Eminem Emmanuel Adebayor Emmanuel Mbasha Enos Olik Entertainment EPL Eric Omondi ESCROW Esma Platnumz Ethiopia Etihad Europe Evander Holyfield Events Exclusive Ezden Ezekiel Wenje Facebook Fadhili Awadh Fahyma Faiza FALLY IPUPA Fashion Fast & Furious Fast &Furious 7 Fast And Furious 8 Ferouz Fetty Feza Kessy Fid Q Fiesta 2013 FIESTA 2014 FIFA Filikunjombe First Godfrey Flaviana Matata Flora Mbasha Florah Mvungi Floyd Mayweather FM Academia Footballer Forads Forbes Fred Swagg Freeman Mbowe freemason freemason tanzania French Montana FUMANIZI Fuse ODG Future JNL G Nako G-Nako GABO ZIGAMBA Gadner Habash Galaxy Glass Gari Inauzwa gari mpya Geez Mabovu Gelly wa Rhymes GENEVIEVE Gentriez ghana Ghetto Kids Gift Gigy Money Girls global publisher Gmail Gnako Godbless Lema Godfather Godzilla Goodluck Gozbert Google Google Glass Gospel Gossip Grace Msale gwajima H BABA Habari Hakeem 5 Halima Kimwana Halima Mdee halimaty msodoki HAMISA MOBETO Hanscana Happiness Watimanywa Haristot Shungu Harmonize Harusi Hasheem Thabit Health Hemedi Hemedi Suleiman "PHD" Hillary Clinton Hip Hop HiPipo Awards HollyWood Homa La Jiji Hot In Town hot photo How To How to Love HTC Huddah HUSNA HUSNA MAULID Hussein Machozi Ian Ferrao Ice Prince Idris Sultan Imetosha Imetosha Campaign India Injili Instagram Interview iPhone iPhone 6 News iPhone 7 Irene Paul Irene Uwoya Iringa Isabela Issaya Mwita Charles Ivan Don Iyanya Izzo Business jack Cliff Jack Pemba Jackline Wolper jaguar Jah Prayzah Jakaya Mrisho Kikwete Jambo Squad Jamii January Makamba jaraja kubomoka jason deruLo jason deruro Jay C Jay Z JB Jini Jini Kabula Joh Makini Johari JOHN CENA John Legend john lennon John Mnyika John Woka Johnnie Walker Jokate jomo kenyata jordin sparcks Jose Mourinho Joseph Mbilinyi Joseph Msukuma Joti Joyheart Events JPEG Jude Okoye Juma Kaseja Juma Nature Jussie Smollett Justin Beiber Justin Bieber Jux K Lyamo K-LYN K.O K’naan kajala Kala Jeremiah Kalakala Kamikaze Kanga Moko Kanumba KANUMBA DAY Kanye West Karrueche Kassim Majaliwa Kayumba KCEE KCMC keisha Kelly Rowland Kenya kenya celebs Kesi Kevin-Prince Boateng Khadija Kopa Kiba Square Kidoa Kifo kigamboni Kigwangalla kikwete Kili Home Kilimanjaro Kilimanjaro Premium Lager Kim Kardashian Kimbunga Mchawi King Crazy GK King Kaka King Lawrence king majuto Kingunge Kitale Kizz Kiduku Klyn Koffi Olomide KOREA KR Mullah KTMA Kubenea kujinyonga kujiua Kupatwa Kwa Jua Kush Tracey Kutongoza Kylie Jenner LAANA LADY GAGA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lagos Laveda Le Mutuz leo Leo Mysterio Life Style Lij Michael LIL DRAINO lil kim Lil Wayne Linah Linex Lira Galore Live Updates Liverpool LOL Lola-Rae Lord Eyes Lost Airplane Love Love And Relationship Love Matters Love Story Love Tips Love Zone Lucci Luis Figo Luis Munana Lulu Lulu La Diva Lundenga Lupita Nyong'o Lynn M-Pawa M-Pesa m-rap MAAJABU Maalim Seif Sharif Hamad Mabeste MABOMU Mabruki Madam Rita Madawa ya Kulevya madee mademu Madhara Ya Mafikizolo MAFURIKO YA MAJI mafuriko ya mvua Magari Mazuri magazeti maimartha jesse Mainda Maisha Majanga Majay Makala makalio Makamba makavu live Make Love Makomando Malaika Malawi Malaysia malaysia airlines Malia Obama Malkiz MAMA DIAMOND MAMA KANUMBA Mama Lulu mama sharo milioneo Mama Wema Man Fongo Man u Man Utd Manchester City Manecky Mange Kimambi mangwea Manji Manny Pacquiao Mapenzi Maphorisa marilyn monroe Mario Balotelli Mark Zuckerberg Markson Beauty Products Marlaw Maromboso martin kadinda Masanja mkandamizaj Mashabiki masoud kipanya Mastaa Mastaa Bongo Master J matako bandia matokeo Matokeo Form Six Matokeo Kidato Cha Nne 2013 Matokeo Kidato Cha Nne 2015 Matonya MATUKIO Maua Maua Sama mauaji maximo MAYA Mayunga MB Dog mbagala Mbeya Mbinu Za Mapenzi MBWA WA WEMA Mc Dulla Mch. Christopher Mtikila Mechi Medicine Meek Mill Mekstar Melania Trump Menina Meninah Mesen Selekta Messenger Messi Mgomo Mh Job ndugai Mi-Casa Micah Boy Michael Jackson Michelle Obama Michepuko Michezo Mike Scotter Mike Tyson milipuko Millard Ayo Millen Magese Mimba Mirror Miss Bongo Movie Miss Bongo Muvi Miss Kilimanjaro 2016 Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 Miss KK Miss Rwanda Miss Tanzania Miss Tanzania 2014 Miss Uganda Miss World misukule Mkasa Mkasi mke wa sugu Mkubwa Na Wanawe Mkude Simba Mlela Mlimani City Mo Dewji mo music Mobile App Model Classic Models moe musa monalisa morogoro Mose Iyobo Moshi Movie Moyo Tara Flavour mpira Mr Blue Mr Flavour Mr Nice Mrema Mrembo Mrembo wa Wiki mrisho mpoto Msaga Sumu Msami Msiba Msigwa Mswaki MTANGAZAJI TIMES FM Mtoto Mtoto Wa Diamond mtoto wa nay wa mitego MTV MTV EMA MTV MAMA MUAJI Mubenga Muchoma Mugabe Muhammad Ali Multichoice Africa Muna Music MUSIC Mustapha Jaffer Sabodo Mwana FA Mwanafunzi Mwanamke MWANZA Mwasiti MZEE GURUMO Mzee Wa Upako Mzee Yussuf Mzee Yusuf Mziiki mzungu kichaa Nafca Nahreel Naj Nakaaya Nald Clever Nameless Nana Kwaku Bonsam NANDO Nape Nnauye Nash MC Nasibu Abdul Juma navy kenzo Nay Wamitego Nazizi Ndege Kupotea ndege ya malaysia Ndikumana Ndoa NEC NECTA Nedy Music Nelly Kamwelu Nelson Mandela Nemo New Blog New Maisha Club new movie New Product new ride New Track New Video News Ney Wa Mitego Neyo Ngasa ngono ya mdomo nguo za kubana Ngwea Nick Wa BongoSwaggz Nicki Minaj Nickson Lema niger celebs Nigeria Nikki Mbishi Nikki wa II Nikki Wa Pili Nisha Nisher Nisher Bye Nisher Entertainment Nissan Note Niva Nixl Carter Nokia Nonini Nora Nuh Mziwanda Nuhu Mziwanda nyerere Nyu Kid Obama Ochu Sheggy Octopizzo Odama Ojwang Olamide Ombeni Sefue Ommy Dimpoz Omotola Omotola Jalade Ekeinde One The Incredible Oprah Winfrey Ordinareh Bingwa Oscar Awards ostaz juma Ousmane Dembele P Diddy P Square P The Mc Pah One pakistan Pam D Pancho Chineke Panya Road Papa Francis Papa Wemba Papaa Masai Papi Kocha Paradise parliament Party Patcho Mwamba Patoranking Paul Kagame Paul Makonda Paul Okoye Paul Pogba Paul Walker Paula Penny Perfect Internet Peter Msechu Peter Okoye Petit Man Photo Photo Of The Day Picha picha za uchi picha chafu picha kli Picha Program Picha Ya Picha za mastaa Picha Za Matukio Picture pingu Pipi Pitbull PNC Political Issues Politics pombe Prezzo Princess Tiffah Privacy Priyanka Chopra Producer Prof. Ibrahaim Lipumba Profesa Jay Promo Promotion Q Boy Q Chief Queen Darleen Queen Darling Quick Rocker R.I.P Raila Odinga rally Rama Dee Rammy Galis Range Rover Sport Raph Tz Ray Ray C Ray Vanny Raymond Rayuu RayVanny Read Madrid Real Madrid Recho Reekado Banks Regina Lowassa Reginald Mengi Rehab Relationship REMIX Rich Mavoko Rich People Richard BBA 2007 Richie Rick Ross Ridhiwani Kikwete Rihanna Rijo Voive RISPER Riyama Robin Thicke Rolene Strauss roma mkatoliki Romeo Romy Jons Rosa Ree Rose Muhando Rose Ndauka Rossie M Rostam Aziz Ruby RunTown Rwanda Sabby Sad News Saed Kubenea Safari Lager said fella Saint West Salam Tmk Salama Condom salama jabir Salamu Tmk Salha Israel Sallam Sk Salman Khan Salomon Kalou Sam Misago samaki wa ajabu Samantha Samatta SamBoy Samsung Samsung Galaxy S5 samweli sita Sarkodie Sasha Obama Sauda Mwilima Sauti Base Sauti Sol SBL sean kingston Secky Seki Selena Gomez Seline Selling Child Senga Serengeti Sergio Agguero Sergio Aguero Serikali Sexy Seyi Shay Shaa Shababi Shamsa Ford SHAMSA SORD Share SHARLEEN Sharo Millionea Sheddy Clever Shein Sherry Zuu Sheta Shetta Shevchenko Shilole Shocking News Sholo Mwamba Show Siasa SIKU KUU YA WAJINGA Simba Simulizi Sintah Siri Ya Mtungi Sitti Mtemvu Siwema Skendo snake bit Snoop Dogg Snura SOAP soccer Social Matters Social Networks SOKO LA KARUME Solution Somalia Somo Songa Sonko Sony South Africa spark Sport News Stamina Stan Bakora Stand United Stanna Stereo Steve Nyerere Steve RnB Steven Nyerere Stone Bone Stori Stori za Bongo Story Lounge suarez subaru Subaru Legacy Sudan SUGU Sumaye Super Nyota 2013 Swahili Jokes Swahili Music T-Pain T.I tahadhari Tajiri Talents Tamthilia tancredo neves tanesco Tangazo Tania tanz TANZANIA Tanzania Film Tanzania Music Tanzania News Tanzania One Tanzanian Tanzanian Actress Tanzanian music Tanzanian Rapper Tayo Folarin TB Joshua TBC Fm TBT TCRA TCU Teachers Technology Tecno Tekno Miles temba Tembo Tetesi TFF Thado The Game The Industry The Next Billionea Thea THT Tiara TID Tiffah Tigo Tiko Timbulo Times Fm Tinashe tip top connection Tiwa Savage tmk Togo Tottenham Hotspur Touch Phone TRA Trace TV trafiki trey songz Trick And Tips Tricks Tros Machine Trubadour George True Story Trust Trust Life TSH to USD Tuddy Thomas Tumaini University Tunda Tunda Man Tundu Lissu Tunisia Tupac Tusker Tuzo Tuzo za watu 2014 Twenty Percent Twerk Video Twitter Tyga U Heard ubakaji UCHAGUZI 2015 Uchawi Uchumi Supermarket ud Udaku Udaku Bongo Udaku Wa Bongo UDOM Uganda ugomvi ugomvi wa wema na kajala Uhuru Uhuru Kenyatta Uhusiano ukatili UKAWA Ukwa Umalaya UNESCO University News Unyama Urembo USA USA Celebs usagaji Usain Bolt Ushauri Usher Raymond Ushoga uswahilini uswazi Utabiri utajiri Utamu Vai Wa Ukweli Valentine Valentine's Day Van Persie Van Vicker vanessa chettle Vanessa Mdee Vannesa Mdee Venezuela VENGU VERA SIDIKA Vicent Kigosi vicent nyerere Vichekesho victoria kimani Video video queen Videos Vin Diesel visa vya mapenzi Vituko Vj Adams VJ Penny Vodacom vurugu Wahu WAJE Wale Walter Chilambo Wanawake Warning wasanii Wasira wastara Wayne Rooney wazungu WCB Wasafi Wedding Wedding Tanzania Weight Loss Welu Sengo WEMA Wema Sepetu wema sepetu alia wema sepetu kuzaa wema sepetu na ugumba Westgate Weusi Whatsapp Wildad William Bugeme Windhoek Beer Wise De Africa Wise One Witchcraft Witnesz wiz khalifa wizi Wizkid Wonder World News World Record Yamoto Band Yanga Yasinta Ycee Yemi Alade yesu bandia YMCMB Young D Young Dee: Situmii Madawa ya Kulevya ila Napiga Mtungi Kwa Sana Young Killer Young Money Yoweri Museveni yuzo mkali yvone chakachaka Z Anto z-anto zamaradi mketema Zanzibar Zari Zari All White Party Zari The Boss Lady Zimbabwe Zitto Aama Chama zitto kabwe Zitto Kabwe ACT Zlatan Ibrahimovic Zuhura Gora Zuleha Zuzu
false
ltr
item
BongoSwaggz.Com : Exclusive: Mastaa 15 wenye nguvu zaidi Afrika Mashariki – 2015
Exclusive: Mastaa 15 wenye nguvu zaidi Afrika Mashariki – 2015
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/07/1555.jpg
BongoSwaggz.Com
http://www.bongoswaggz.com/2015/07/exclusive-mastaa-15-wenye-nguvu-zaidi.html
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/
http://www.bongoswaggz.com/2015/07/exclusive-mastaa-15-wenye-nguvu-zaidi.html
true
371784233821042440
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy