Advert

Breaking News

Senga: Busu la Kajala Lilinifanya Nilale Usingizi Mnono

Staa wa vichekesho kutoka Bongo Movies, Joseph Senga ‘Senga’ amefunguka kuwa busu alilompiga staa wa kike wa filamu, Kajala Masanja lilimfanya alale usingizi mnono sana ukizingatia kuwa hajawahi kubusu shavu laini kiasi hicho kwasababu warembo wengi wanazingua.
Senga: Busu la Kajala Lilinifanya Nilale Usingizi Mnono
Akizungumza na GPL, Senga alisema alipata fursa hiyo ya kumpiga busu wakati wakiigiza filamu matata ya Pishu iliyoandaliwa na Kajala Entertainment, itakayoingia sokoni Mei Mosi, ambapo alisema anajikubali katika filamu hiyo ambayo anaamini itavunja watu mbavu.

“Wewewee umpige busu Kajala utashindwa kulala kweli jamani,yaani nilishtuka kumeshakucha kabisa lakini pamoja na yote mimi ni mchekeshaji ila kwa filamu ya Pishu nimeinua mikono,” alisema Senga.
-GPL
KWA VIDEOS ZA MASTAA WA BONGO NA VITUKO KUTOKA BONGO SWAGGZ TV, BOFYA HAPA Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.